Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA YA GESI WATAKAOFANYA UDANGANYIFU KWENYE UZITO WA MITUNGI YA GESI KUTOZWA FAINI

 


Wakala wa Vipimo Mkoa wa Mwanza, imewataka wauzaji na wasambazaji wa nishati ya gesi kutumia mizani sahihi iliyohakikiwa na wakala huo ili kumlinda mlaji pamoja na kuepusha usumbufu dhidi yao ikiwemo kutozwa faini  isiyozidi shilingi milioni 20 kwa kosa la udanganyifu wa uzito kwenye mitungi ya gesi.


Onyo hilo limetolewa na meneja wa wakala wa vipimo mkoa wa Mwanza Hilolimus Mahundi katika kikao cha kuwajengea uelewa wadau wa biashara ya gesi ili waweze kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo kwa ajili ya kumlinda mlaji wa mwisho asipate kipimo pungufu katika mitungi ya gesi



Baadhi ya wauzaji na wasambazaji wa mitungi ya gesi kanda ya ziwa wakizungumza baada ya kikao hicho, wameahidi kufanya biashara zao kwa uaminifu na uadilifu ili kumfanya mlaji wa mwisho aone faida ya kutumia nishati ya gesi.



Meneja wa wakala wa vipimo mkoa wa Mwanza Hilolimus Mahundi amewaonya tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wa bidhaa za vyakula kuacha tabia ya kujaribu kuchezea mizani kwa lengo la kuwaibia wateja akisema watakaobanika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI