Header Ads Widget

"ASILIMIA 98.04 ZA SAMPULI ZAKIDHI VIWANGO"_TPHPA

 




Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


JUMLA ya  Sampuli 1025 za Viuatilifu zimefanyika, ambapo sampuli 1005 sawa na asilimia 98.04 zilikidhi viwango ,huku sampuli 20 sawa na asilimia1.96 hazikukidhi lengo likiwa ni uhakiki wa ubora


Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru wakati alipokuwa akieleza utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita.


Amesema  Mamlaka imeendelea kufanyika kaguzi ili kupunguza uwepo wa viuatilifu bandia,ambapo jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji 198 vilisajiiliwa.


"Lakini pia vibali vya shehena za viuatilifu 1324, ujazo wa lita 58,379,97.98 na kg 3,880,772.77, mapato kiasi cha bil.3.06 nakusema kuwa jumla ya vibali vya maduka 802 vilitolewa kwa wafanyabiashara wa viuatilifu," Amesema 


Hata hivyo ametaja changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni pamoja na uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, elimu juu ya visumbufu na namna ya kudhibiti,lakini pia kumekuwepo na wauzaji wa viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu.


Vilevile amesema kuwa malengo ya TPHPA ni pamoja na kuendelea kuwajengea uwezo wataalamu wa mamlaka katika kusimamia na kudhibiti milipuko ya visumbufu kwa wakati.



Pia amesema malengo mengine kutumia “DNA technology” katika kutambua aina za wadudu na magonjwa ya mazao ili kuwa na udhibiti endelevu, Kuweka mfumo wa ufuatiliaji wa viashiria (early warning system) vya uwepo wa mlipuko wa visumbufu.


Kuendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara viuatilifu kwa watengenezaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji ili kupunguza athari ya kuwepo kwa viuatilifu bandia. 


"Katika kipindi hiki, mamlaka inafanya ukaguzi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha,Manyara, Mbeya, Njombe, Iringa, Songwe, Morogoro,Mbeya" amesema


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI