UONGOZI mzima wa timu ya Yanga Sc ukiongozwa na Rais wa timu hiyo Eng.Hersi Saidi na Msemaji wa timu hiyo Ally Kamwe wametembelea hospitali ya taifa Muhimbili Mloganzila na kutoa pole ya wagonjwa katika Hospitali hiyo leo tarehe 5/3/2023 jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wanahabari wakati wa utoaji wa zawadi hizo Rais wa timu hiyo amesema wamekuja hapa katika Hospitali ya taifa ya mlonganzila kutoa pole kwa mfanyakazi wa timu hiyo ambaye anaumwa na amelazwa katika Hospitali hiyo Dada Elvina.Lakini pia kutoa zawadi za pole kwa wagonjwa wote wa ambao wapo katika Hospitali.
" Tupo hapa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila kwa matukio mawili moja kumtembelea mfanyakazi wa Young Africans ambaye yupo hapa amesumbuliwa na ugonjwa kwa muda mrefu lakini pia kutoa zawadi kwa wagonjwa ambao wapo katika Hospitali hii ya mlonganzila," Amesema Eng.Hersi Saidi Rais wa Yanga Sc.
Naye,Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Julieth Magandi ameongea na kutoa pongezi kwa uongozi mzima wa timu ya taifa Muhimbili Mloganzila ametoa shukurani zaidi kwa moyo ambao uongozi wa timu ya yanga umeonyesha kwa kujali na kurudisha kwenye jamii."Amesema Julieth Magandi Naibu mkurugenzi Hospitali ya taifa Mloganzila.
0 Comments