Mkurugenzi wa shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisheries Development Bwana Edwin Soko ametembelea mwalo wa Muswahili uliopo Jijini Mwanza eneo la Mkuyuni ili kuona changamoto inayoikabili sekta ya uvuvi
Baadhi ya wavuvi katika mwalo wa Mswahili Jijini Mwanza wamekili uwepo wa changamoto katika sekta hiyo na kuomba Serikali kutoa elimu kuelimisha kufanya uvuvi salama ikiwemo mbinu za kuogelea pamoja na matumizi sahihi ya lifejackets
Mwenyekiti wa vikundi shirikishi katika mwalo wa Muswahili Jijini Mwanza Robert Charles amesema, suala la usalama kwa wavuvi ziwani linatakiwa kuwa endelevu kutokana na baadhi kutozingatia elimu inavyotakiwa na vitendea kazi ikiwa changamoto kubwa
Katika hatua nyingine Soko amesema, kuna uitaji mkubwa kwa wavuvi wanapofanya shughuli zao ikiwa ni mafunzo ya kutumia viokozi ( Lifejackets ) wengi wao kuonyesha uitaji mkubwa na tunaiomba Serikali kutatua changamoto hizo
0 Comments