Header Ads Widget

MBUNGE ANNE KILANGO ATOA MSAADA WA KITIMWENDO.



NA WILLIUM PAUL, SAME.


MBUNGE wa Jimbo la Same mashariki mkoani Kilimanjaro, Anne Kilango Malecela amekabidhi msaada wa kiti mwendo kwa mtoto Ally Ramadhani (6) ili aweze kukitumia kwenda shule.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo ambaye aliikabidhi familia hiyo jana Ndungu alisema kuwa, alipigiwa simu na mama mzazi wa mtoto huyo, Agness Elifuraha na kumweleza kuwa anamtoto mlemavu ambaye hawezi kutembea.



Anne Kilango aliendelea kudai kuwa, mama huyo alimwambia kuwa mtoto wake amefikia umri wa kuanza shule lakini anashindwa kwenda kumwandikisha na kumpeleka shule kutokana na kukosa kitu mwendo na kumuomba aweze kumsaidia kupata kiti mwendo.

Akieleza kwa uchungu huku akibubujikwa na machozi mama mzazi wa mtoto, Agness alisema kuwa,kila siku Ally amekuwa akimsumbua kutaka kwenda shule lakini walishindwa kumpeleka kutokana na hali aliyokuwa nayo.


Agness alisema kuwa, kupata msaada wa kiti hicho kutoka kwa Mbunge sasa ataenda kumwandikisha shule mtoto huyo kwani atakuwa akikitumia kiti hicho kwenda na kurudi shule.



"Ninayofura kubwa sana leo kuona ndoto ya mtoto wangu kusoma sasa itatimia kwani kilichokuwa kikimkwamisha kusoma kilikuwa ni kiti mwendo sasa leo hii amekipata" alisema Agness.

Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI