Na Amon Mtega_Mbinga.
KATIKA utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM Mamlaka ya ukusanyaji wa mapato (TRA) ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma imeweza kufikia asilimia 81 ya makusanyo kwa kipindi cha miezi sita Julai hadi Disemba 2022.
Akizungumzia mafanikio ya ukusanyaji wa mapato hayo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM, Meneja wa TRA Wilaya ya Mbinga Kitalile Angetile amesema kuwa mafanikio hayo yanapatikana kutokana na baadhi ya walipa kodi (Wafanyabiashara)kutambua umuhimu wa kulipa kodi.
Angetile ambaye pia taarifa hiyo imewasilishwa kwenye Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya hiyo ya CCM ya kupokea utekelezaji wa ilani kutoka Serikalini.
Meneja huyo amesema kuwa licha ya mafanikio hayo lakini bado TRA Wilayani humo imeweza kuwapatia namba ya mlipakodi kwa Wafanyabiashara 578 katika kipindi cha Julai 2022 hadi Desemba 2022 jambo ambalo amesema linaonyesha mafanikio juu ya walipakodi hao.
Amefafanua kuwa Elimu dhidi ya mlipakodi kulipa bila kufanyiwa msukumo inaendelea kutolewa ili Mwisho wa siku kila mmoja aone umuhimu wa kulipa kodi kwa kuwa kodi hizo ndizo zinazosaidia kutekeleza miradi mbalimbali kwa kusimamiwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan .
0 Comments