Header Ads Widget

RPC - RUVUMA AWANYOOSHEA KIDOLE WATU WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VIOVU KWENYE JAMII.

 


          Na Amon Mtega _Ruvuma.

KAMANDA wa Polisi Mkoani Ruvuma ACP Marco Chilya amewataka watu wanaofanya vitendo viovu (Wizi) kwenye jamii kuacha tabia hiyo  kwa kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo limejipanga vema kukabiliana na waovu hao.


Kauli hiyo ameitoa wakati akitoa taarifa ya ufanyaji kazi wa Jeshi hilo ambapo ndani ya mwezi mmoja limefanya msako na kufanikiwa kuvikamata vitu mbalimbali vikiwemo vilivyoibiwa kwenye makazi ya watu.



Kamanda Chilya amesema kumekuwepo na baadhi ya watu wanaofanya vitendo viovu kwenye jamii huku wakiamini kuwa hawatakamatwa jambo ambalo amesema wanajidanganya kwa kuwa Jeshi la Polisi lipo imara na lipo kazini muda wote.


 Akizungumzia mafanikio ya msako wa mwezi mmoja amesema kuwa Jeshi hilo limekamata meno ya Tembo mazima 13 na vipande 13 jumla yakiwa meno 26, jino moja la Kiboko,Nyama ya Nguruwe pori vipande 08 ,Miba ya Nungunungu ,Nyama ya Mbalahapi vipande 34, Nyama ya Pofu vipande 70 na Nyama ya Ngorombwe.



Chilya amesema katika msako huo wamekamata silaha 03 ambapo 02 aina Gobole ambazo zinadaiwa zimekuwa zikitumika katika shughuli za ujangiri huko katika Wilaya ya Nyasa na Tunduru na pia katika maeneo ya Tarura Wilaya ya Songea imeokotwa silaha 01 aina ya Short Gun yenye namba za usajili TZCAR34047 iliyokuwa imetelekezwa na kuwa mtuhumiwa aliyetelekeza silaha hiyo ambaye anadaiwa kuwa mlinzi wa kampuni ya Buchosa amekamatwa kisha kufikishwa Mahakamani hivyo Jumla ya watuhumiwa 03 na silaha 03 kukamatwa.


  Aidha kamanda huyo amesema kuwa katika msako huo uliofanyika katika maeneo mbalimbali ya Mkoani humo wamekamata   Pikipiki 19 , Screen zenye ukubwa tofauti zipatazo 75 ,mafuta ya Diesel lita 1290,Magodoro 06 aina ya Super Banco /Tanform na kuwa wamekamata madawa ya kulevya (BHANGI) kilo 09 na gramu 865, Miche ya bhangi 851, Mbegu za bhangi kg 450 ambapo jumla ya kesi 16 za madawa ya kulevya aina ya bhangi zimefikishwa Mahakamani watuhumiwa 33 wamekamatwa ambapo watuhumiwa 12 wameshafikishwa Mahakamani.



Pia Jeshi la Polisi Mkoani humo limekamata pombe Moshi , Jumla ya lita 178, mililita 216 za pombe moshi (Gongo) mitambo 09 ya kutengenezea pombe hiyo imekamatwa na watuhumiwa 31 wameshafikishwa Mahakamani kwa hatua za kisheria.


Kufuatia masako huo kamanda huyo amewataka wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kwenda kuzitambua mali zao walizoibiwa ikiwemo , Pikipiki, Screen na Magodoro katika kituo kikubwa cha Polisi kilichopo Mjini Songea.

       


    

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI