Na Amon Mtega, _Mbinga.
MBUNGE wa Jimbo la Mbinga Vijijini Benaya Kapinga ametumia usafiri wa pikipiki ya mairi matatu(Bajaji) katika kuzungukia maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwaungamkono Vijana wajasiriamali kwa kufanya kazi hiyo.
Mbunge huyo amesema kuwa ameamua kutenga muda mchache wa kutumia usafiri wa Bajaji na kuliacha gari lake la kibunge kwa lengo la kuungamkono jitihada za ujasiliamali zinazofanywa na Vijana hao.
Aidha Mbunge Benaya amewapongeza Vijana wanaojishughulisha na ujasiliamali huo huku akiwataka waendelee kuwa na weledi katika kazi hiyo kwa kuwa ni sehemu ya ajira huku akisema Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inazidi kuweka mipango mizuri kwa Vijana wanaojituma kufanya kazi.
Benaya ambaye ameongozana na baadhi ya wajumbe wakitumia usafiri wa Bajaji hiyo amesema kuwa Jimbo la Mbinga Vijijini na Jimbo la Mbinga mjini ni majimbo ambayo baadhi ya changamoto zinalingana kwa kuwa watu wanaohudumiwa ni wamaeneo yanayofanana .
0 Comments