Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
KATIKA kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022 Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limepokea na kushughulikia malalamiko takribani 369 ya Uchafuzi na Uharibifu wa Mazingira kutoka kwa wananchi.
Malalamiko hayo nipamoja na kuvuja kwa mafuta kutoka kwenye mabomba ya mafuta ,kuchoma taka hatarishi chini ya kiwango kinachotakiwa kisheria.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo Dkt. Samwel Gwamaka ameeleza hayo leo jijini hapa wakati akieleza mafanikio ya Baraza hilo katika kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa serikali ya Awamu ya Sita.
" Malalamiko hayo yalihusisha uchafuzi wa vyanzo vya maji, utiririshaji wa maji taka ,uchafuzi wa hewa kutokana na shughuli za viwandani,kelele za muziki,kushamiri kwa gereji bubu maeneo ya makazi,kushamiri vituo vya mafuta katikati ya makazi ya watu,matumizi ya mifuko ya plastiki iliyokatwa na kutapaka maeneo ya makazi na kuhakikisha inatoa elimu elimu sahihi na suluhisho juu ya jambo husika," Amesema Mkurugenzi Gwamaka
Hata hivyo Mkurugenzi huyo Dkt Gwamaka amesema Baraza limefanikiwa kusajili miradi 1702 ambapo kati yake 967 ni ya {TAM} na 735 ni ya ukaguzi wa Mazingira.
Aidha Kwa kupitia taarifa ya Tathimini ya Athari kwa Mazingira katika kipindi cha Julai 2021 hadi Februari 2022 Baraza limefanikiwa kusajili miradi 1702 ambapo kati yake 967 ni ya (TAM)na 735 ni ya ukaguzi wa Mazingira
Dkt.Gwamaka ameeleza kuwa Baraza hilo limetoa Jumla ya Vibali 174 vya kushughulika na taka hatarishi ndani ya Nchi ambapo vibali 10 vya kuingiza na kusafirisha nje ya Nchi na kupelekea kiasi cha Tani 516,041 za taka mbalimbali kukusanywa na makampuni yenye vibali.
"kukusanywa huku kwa tani 516,041 za taka inaonesha jinsi Braza linavyowajibika katika kuhakikisha Sheria ya Mazingira inayozingatia uhifadhi na utunzaji wake unazingatiwa na ndio maana pia tumetoa jumla ya vibali 174 vya kushughulika na taka hatarishi ndani ya Nchi yetu .
Hata hivyo amebainisha usimamizi wa tafiti za Mazingira huku ikifanikiwa kuratibu uteuzi wa Eneo la Rufiji-Mafia-Kibiti-Kilwa {RUMAKI} ikiwa na lengo la kujumuishwa katika mtandao wa kidunia wa Hifadhi za Binadamu na Hifadhi hai.
0 Comments