Na:Dickson Bisare Matukio Daima TV Dar es salaam.
Bodi ya Baraza la Michezo Tanzania likiongonzwa na Mkurugenzi wa michezo ya maendeleo Tanzania limekabidhi bendera kwa mwanamichezo wa aina ya Pooltable katika ukumbi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) leo tarehe 17/3/2023 uliopo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wanahabari wakati wa utoaji wa bendera hiyo Mkurugenzi Ally Mayaye Tembele Mkurugenzi ameanza kwa kumpongeza kijana na mwakilishi pekee mtanzania ambaye ameweza kudhubutu kwa kuweza kudhubutu kucheza katika mchezo huo wa pooltable hakika kama nchi ni heshima kubwa ambayo sisi kama taifa la Tanzania tunaenda kulipata.
Ameendelea mbele kwa kusema kwamba kwa utubutu wenu nawapongeza sana kwa hili na ninamaani kwa uzoefu ulionao unaenda kurudi na ushindi mkubwa na ninaimani na wewe na taifa linaimani na wewe,na Serikali ya Jamhuri wa Tanzania milango wa utamaduni Sanaa na michezo ipo wazi kuweza kuipa sapoti michezo kwa muda wowote ule."
Naye,Mwenyekiti wa kamati Hamasa Raphael Mathias Mroso(Mwakilishi wa Rais wa Mchezo wa Pooltable) Isack Togoto wakati anaongea na wanahabari katika ukumbi wa BMT uliopo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa amesema.
"Sisi Chama wanachama wa mchezo wa pooltable,lengo la sisi kuwepo hapa ni kuomba ridhaa kwa kukabidhiwa bendera kwenda kuliwakilisha taifa huko nchini China.Kama Tanzania sisi ni wadau wa mchezo wa pooltable tulipata mualiko huu kutoka kwa baraza la Michezo wa Tanzania kuweza kuja kupokea bendera kwa ajili ya kuliwakilisha taifa nchini China kwenye mchezo wa pooltable."
Sambamba na hiyo ndugu Mroso ameenda mbele na kusema Tanzania katika mchezo wa Pooltable ni nchi pekee ambayo imewahi kushiriki katika mchezo huu wa pooltable na nina Imani kubwa na ndugu Abdalla Hussein Abdallah (Mchezaji wa Mchezo wa Pooltable)anaenda kufanya vyema na mchezo huo unaenda kuanza tarehe 20 March hadi 20 April,2023 ambapo wanatakiwa kuanza safari yao leo jioni.
Naye,Ndugu Abdallah Hussein Abdallah wakati wa kujibu baadhi ya maswali ya wanahabari ameweza kuongea na kutoa utayari wake kuelekea mchezo wake unaoenda kufanyika nchini China,kuweza kuelezea taifa mbele ya vyombo vya habari amesema ana amini kila kitu kitaenda kuwa sawa kuwa na Imani kubwa kwamba anaenda kufanya vizuri kuweza kuliwakilisha taifa vyema kwenye mchezo wake wa Pooltable ambao unaenda kufanyika huko nchini China.
"Mimi nimejipanga vizuri na niwaombe watanzania wenzangu muendelee kuniombea na hakika naamini Katika kupata nafasi hii ninaenda kufanya vizuri kwenye michuano hii na kuweza kurudi na ushindi." Alisema Abdallah Hussein Abdallah Mchezaji wa Pooltable.
0 Comments