Na:Dickson Bisare Matukio Daima TV Dar es salaam.
KOCHA mkuu wa timu ya Simba sc amelezea mandalizi yake kuelekea mchezo wa kesho wa Kimataifa wa Klaby Bingwa Barani Afrika dhidi ya timu ya Horoya Sc mchezo unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi tarehe 18/3/2023 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa mikutano ya wanahabari (Media Centre) kocha mkuu wa timu ya Simba Sc ameelezea maandalizi yake pamoja na wachezaji wake walivyojiandaa kuelekea mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumamosi tarehe 18/3/2023 kuanzia saa moja kamili usiku dhidi ya timu ya Horoya Sc ya kutokea nchini Guinea.
"Mimi kama kocha wa Simba Sc nafahamu kwamba mchezo wa kesho utakuwa mchezo muhimu na mgumu kwangu lakini naamini kwamba kwa maandalizi yangu niliokuwa nao pamoja na timu yangu kambini,kwani mchezo wa kesho ni mchezo ambao Timu yangu inahitaji pointi tatu tu ambazo ni muhimu ili niweze kuvusha timu kwenye hatua ya roo fainali." Roberto Oliveira Kocha mkuu wa Simba Sc.
Huku hayo yakijiri, kocha huyo ameendelea mbele kwa kuendelea kujibu maswali ya wanahabari kocha alijibu swali kutoka kwa mwanahabari ambalo linahusika na Simba kuweza kuingia hatua ya robo fainali kwa takribani michezo yote ambayo timu hiyo imeweza kuingia..Kocha Roberto Oliveira alisema...
"Nafahamu kwamba timu ya Simba Sc kwa miaka yote ambayo imeingia hatua ya robo fainali imekuwa na kocha wenye ubora na mimi naamini ubora wangu utaweza kuivusha timu ya Simba sc kuweza kuvuka hatua ya robo fainali na lazima tutaingia tena kwa mara nne mfululizo hapa hapa nyumbani."
Naye,Mwaakilishi wa wachezaji wa timu ya Simba Sc Shomari Kapombe amezungumza mbele ya wanahabari kujibu baadhi ya maswali ambayo ameulizwa kuelekea matarajio yao wao kama wachezaji kwa ujumla kwani mchezo wa kesho kwao kama timu wanadeni kubwa kwa taifa Lakini pia timu kwa ujumla kuweza kuhakikisha wamevuka wameingia hatua ya robo fainali.
" Kwanza kabisa nianze kwa kusema kwamba sisi kama timu kwa ujumla tumejiandaa vyema na tunafahamu umuhimu uliopo kwetu na kwa taifa kwa mchezo wa kesho hivyo basi,sisi wachezaji tutahakikisha kila kitu kitaenda sawa kulingana na maelekezo ambayo mwalimu wetu ametupa kwa muda ambao tumekuwa kambini kwenye maandalizi kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Horoya Sc.
Hatuwezi kuwa dharau wageni wetu wa Horoya Sc kwani na wao mchezo kesho utakuwa wa umuhimu kwao,lakini sisi kaka wachezaji wa Simba Sc tutatumia faida ya nyumbani kuweza kuhakisha kila kitu kimebaki hapa hapa nyumbani na alama zote tatu ambazo zitatuwezesha sisi kuingia hatua ya robo fainali." Alisema Mwakilishi wa wachezaji wa timu ya Simba Sc Shomari Kapombe.
Kwa kutambua umuhimu wa mchango wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kiasi cha fedha ambazo amezitoa kama Motisha kwa timu zote mbili za Tanzania Simba Sc na Yanga Sc wanaoshiriki michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika lakini pia Kombe la Shirikisho Barani Afrika Shomari Kapombe alikuwa na haya kusema.
" Tunamshukuru sana Mama yetu Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kufahamu umuhimu wa mpira wa miguu katika nchi yake,na kuweza kutoa kiasi cha fedha shilingi milioni tano kwa kila goli ambalo litakuwa linapatikana (Motisha) sisi kama timu kwa ujumla hatutamuangusha tutapambana kwa kila tuwezavyo ili kuweza kuitangaza nchi yetu vyema Kimataifa." Alisema Mwakilishi wa wachezaji wa Timu ya Simba Sc Shomari Kapombe.
0 Comments