Header Ads Widget

ASKOFU WA KKKT RUVUMA AONGOZA IBADA YA KUAGA MWILI WA COSTANTINO NZIKU .

 


Na Amon Mtega, Songea

ASKOFU wa Kanisa la Lutheran Dayosisi ya Ruvuma Amon Mwenda ameongoza ibada  ya  kuuaga mwili wa mfanyabiashara Costantino Nziku(Makabest) aliyefariki dunia Machi 20 mwaka huu.


 Mwenda akiongoza ibada hiyo iliyofanyika  Msamala ambayo imehudhuliwa na mamia ya Wakazi wa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma amesema kuwa mwanadamu anatakiwa akae amejiandaa siku zote kuwa hapa duniani anapita.



 Askofu huyo amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya mwanadamu kujisahau na kujifanya maisha ya duniani ni ya milele kumbe sivyo bali kuna maisha mengine baada ya kutoweka hapa Duniani.


 Akimuelezea marehemu huyo ambaye mwili wake utazikwa kwenye Nyumba ya milele Kijijiini kwake Makambako Mkoa wa Njombe amesema kuwa marehemu alikuwa mcha Mungu ambaye alipenda kufanya ibada licha ya kuwa na shughuli zake za kibiashara.

 

 Askofu Mwenda ambaye alianzisha wimbo wa 205 katika kitabu cha nyimbo na neno la takatifu kusomwa katika kitabu cha Biblia  Mhubiri tatu  mstali wa kwanza hadi wa pili uliibua hisia za waombolezaji wengi ambao walishindwa kujizuia kufuatia marehemu Costantino Nziku kuishi na jamii kwa maisha ya kawaida yakiwemo ya upendo .



 Kwa upande wake mmoja wa Wafanyabiashara Pascal Msigwa(Top one in) wakati akitoa neno la shukurani amesema kuwa familia ya marehemu inawashukuru wote ambao wamejitoa katika kushiriki tukio hilo.



Marehemu Costantino Nziku alizaliwa 1972 na amefariki gafla baada kutoka kufanya mazoezi kwenye mashine yake nyumbani kwake na kuwa alipokimbizwa katika Hospitali ya Songea (Homso)madaktari walidhibitisha kuwa amefariki Dunia.

         


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI