Header Ads Widget

YANGA YAJIDHATITI KUELEKEA MCHEZO WAO NA TP MAZEMBE





Benchi la ufundi la Klabu ya Young Africans limesema  limechukua tahadhari ya kutosha Katika mchezo wao wa kesho dhidi ya TP mazembe, baada ya kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza Katika mchezo wao wa awali walio poteza kwa mabao mawili bila majibu dhidi ya Us monastir Ugenini.



Akizungumza na wanahabari leo  kwenye ukumbi wa Tanzania Football Federation  (TFF) Kocha wa  timu ya Yanga sc Nasdine Nabii  kusema kuwa  anatambua mchezo wao wa kwanza walipoteza dhidi ya US monastir kwa mabao mawili bila na kusema mchezo wa kesho wachezaji wake wapo na kwenye hari kubwa   kwani wanatambua umuhimu wa mchezo wa huo dhidi ya Tp Mazembe.


"Ninatambua kwamba mchezo uliopita tulipoteza,kutokana na makosa madogo madogo ya kimchezo tunatambua mpira wa miguu ni mchezo wa makosa,hivyo basi tumepoteza mchezo uliopita na naamini mchezo wa kesho nimewandaa wachezaji wote japokuwa tutaenda kuwakosa wachezaji watu;Bernard Morrison,Sure Boy na huenda na Stephen aziz Ki ambaye hajawa na match fitness bado tangu tumetoka Tunisia."Nasdine Nabii Kocha Mkuu wa Yanga Sc. 


Naye,mchezaji wa timu ya YangaSc Zawadi Mauya amesema wao kama wachezaji wanajua mchezo wa kesho gautama mchezo rahisi,lakini wao kama wachezaji wamejiandaa na wapo tayari kwenda kuipambania timu na ZaidiTaifa kwa ujumla.


" Mashindano haya kikubwa yanahamasishwa na hamasa,hivyo basi sisi wenyewe kama wachezaji tupo na ari na moyo mkubwa na tunaenda kuhakikisha tumetoka na mchezo wenyewe huo wa kesho."Amesema Zawadi Mauya Mchezaji wa YangaSc.


Mwisho*

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI