Header Ads Widget

“RHINO BOY” APANDA MLIMA KILIMANJARO KUINUA UELEWA DUNIANI KUHUSU MNYAMA FARU ALIYOKO HATARINI KUTOWEKA


Na. Edmund Salaho – KILIMANJARO

Akiwa amevalia vazi kamili lenye muonekano wa mnyama FARU mwanaharakati wa kutunza mazingira kutoka Uingereza na Balozi wa " Save the Rhino International" Chris Green, maarufu kama “Rhino Boy,” amefaulu kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuchangisha fedha na kuhamasisha dunia kuhusu hatari kubwa inayoikabili moja ya wanyama walioko hatarini zaidi kutoweka duniani 

Green aliweza kufanya safari ya kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika unaojulikana pia kama “Paa la Afrika,” wiki hii baada ya safari ya siku sita safari iliyoanza Januari 16, 2026.

Akizungumza na wanahabari Januari 21, muda mfupi baada ya kushuka mlima, Green alielezea changamoto hiyo kama iliyokuwa ikichosha kimwili lakini ikimfariji kihisia.



“Nimetembea hadi kileleni cha Mlima Kilimanjaro na kurudi chini,” alisema. “Kimwili, najihisi kama Faru mchovu kuliko wote. Lakini kihisia, najihisi nikiwa mwenye furaha na tumaini kubwa.”

Tumaini hilo, Green alieleza, lilitokana na ushirikiano mkubwa aliopata katika safari hiyo, wakiwemo maafisa wa Hifadhi za Taifa Tanzania *(TANAPA),* waongozaji, wabebaji  mizigo, na wapandaji wenzake.

“Moyo wangu umejaa tumaini kwa sababu njia pekee niliweza kufanya hivi ni kupitia usaidizi wa watu wa hapa Tanzania,” alisema. “Kila mmoja alishirikiana ili kumsaidia ‘Faru’ huyu kufika kileleni. Hii inaonyesha inawezekana tukifanya kazi pamoja, tunaweza kusaidia mazingira, kusimama kidete kwa ajili ya uhifadhi, na kuokoa Mnyama Faru.



Kupanda Kilimanjaro ni kazi ngumu hata katika mazingira ya kawaida. Jaribio hilo likiwa na vazi zito la Faru linaongeza ugumu wa zoezi hilo kufika kileleni.

“Kila siku mlima ulikuwa mkubwa mno na changamoto ilikuwa kubwa sana,” alisema. “Wakati mwingine ilionekana kama haiwezekani. Lakini hakuna kisichowezekana ukitoa moyo na roho yako yote hasa ukiwa umezungukwa na watu wema.”

Green alisema alipata nguvu kutokana na lengo la kupanda: kuokoa maisha ya Faru. Spishi tano za Faru duniani zimeainishwa kuwa kwenye hatari kubwa ya kutoweka, akiwemo Faru mweusi wa Afrika ambaye bado anakumbwa na shinikizo la ujangili na kupotea kwa makazi.

“Faru wamekuwa ni wanyama ninaowapenda zaidi,” alisema. “ Wanaashiria mambo yote tunayotakiwa kujitahidi kuwa kama binadamu ni wapole, wanyenyekevu, na wakuu. Inaniumiza kuona wako hatarini kupotea. Nilihitaji kufanya hili ili kutoa mwamko kuhusu hali yao, ili pamoja tuweze kuleta mabadiliko.”

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Faru, idadi yote ya spishi zote tano za Faru duniani inakadiriwa kufikia Faru 27,000. Ingawa viwango vya ujangili vimepungua kutoka mwaka mmoja uliopita, biashara haramu ya wanyamapori bado ni kubwa. Nchini Afrika Kusini pekee, angalau Faru mmoja bado wanauawa na majangili kila siku, ikiwa ni wastani wa Faru 420 waliuawa mwaka 2024 na 195 katika nusu ya kwanza ya 2025.




Green alisifia Tanzania na taasisi zake za uhifadhi kwa msaada wao, akizipa Hifadhi za Taifa Tanzania alama ya juu katika kuhifadhi na kulinda rasilimali wanyamapori “kumi kwa kumi.”

“Tangu nilipowasili, nimepokelewa na ukarimu na upendo tu,” alisema. “Wangeweza kupata sababu mia ya kusema hapana, lakini badala yake walitafuta kila sababu ya kusema ndiyo.”

Akihitimisha mkutano na waandishi wa habari, Green alitoa wito kwa dunia kuchukua hatua za pamoja kulinda wanyamapori.

“Ninajihisi kama Tanzania yote iko nyuma yangu na nyuma ya " Save the Rhino" Shirika ambalo najivunia sana kuliwakilisha,” alisema Tukiwa na marafiki kama hawa, kila kitu kinawezekana. Tuwalinde wanyama, tuokoe spishi za Faru.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI