Header Ads Widget

WAKAZI WA MAKATANI MBINGA WAISHUKURU HALMASHAURI YA MBINGA MJI KUTUMIA MAPATO YAKE YA NDANI KUJENGA ZAHANATI.

 


 Na Amon Mtega,  Mbinga.

BAADHI ya Wakazi wa Kijiji cha Makatani kata ya Kagugu Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wameishukuru Halmashauri ya Mbinga mji kwa kutumia mapato yake ya ndani sh.Milioni 26 katika kufanikisha Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho kwa kushirikiana na Wananchi.


Akizungumza mmoja wa Wakazi wa Kijiji hicho Grace Mapunda amesema kuwa kukamilika kwa Zahanati hiyo kutawaondolea adhaa ya kutembea kwa muda mrefu kufuata huduma jambo ambalo limekuwa likiwaharishia maisha.



Mapunda amesema kuwa katika kipindi cha nyuma kabla ya Zahanati hiyo wakinamama wajawazito baadhi yao wamekuwa wakijifungulia njiani pindi wanapofuata huduma ya Hospitali hatimaye baadhi wamekuwa wakikutwa na vifo.


Mwananchi huyo ameishukuru Halmashauri ya Mbinga mji pamoja na Serikali kwa kusaidiana na Wananchi wa Kijiji hicho kukamilisha Ujenzi wa Zahanati hiyo.



Kwa upande wake Afisamtendaji wa Kijiji cha Makatani Subira Komba amesema Zahanati hiyo imekamilika kinachosubiriwa ni ukabilishaji wa vyoo ambavyo tayari vipo hatua za mwisho kukamilika ili Zahanati ianze kufanya kazi ya kuwahudumia Wananchi.


Naye Kaimu Afisa Mipango  wa Mbinga mji Eliudi Ngwavi amesema kuwa Ujenzi wa Zahanati hiyo umetumia nguvu za Wananchi kwenye baadhi ya Ujenzi kama kuchimba msingi na tofali na kuwa Halmashauri imechangia Ujenzi huo kwa mapato ya ndani kiasi cha Sh.Milioni 26.



     

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS