Header Ads Widget

MADIWANI MBINGA WAWATAKA WAKUU WA TAASISI ZA SERIKALI KUJITOKEZA KWENYE VIKAO ILI KUJIBU HOJA

 





Na Amon Mtega_ Mbinga


BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Mbinga mji Mkoani Ruvuma limewaka Viongozi (Meneja) wa taasisi za Serikali kuacha tabia ya kutuma wawakilishi kwenye vikao vya baraza la Madiwani ili kuzijibu hoja mbalimbali za Wananchi zinazoelekezwa kwenye taasisi hizo.


 Akizungumza mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Kelvin Mapunda wakati wa kikao cha baraza hilo la robo ya pili ya mwaka ambapo baadhi ya hoja zimeshindwa kupatiwa majibu baada ya taasisi zinazotakiwa kujibu hoja hizo zimewatuma wawakilishi badala ya Viongozi wao.


Mkutano wa baraza hilo ulipoanza umeanza na baadhi ya taasisi kama Tarura,Tanesco,Mbiwasa  huku wakuu wao kushindwa kutokea kwenye baraza hilo ambapo ni taasisi moja tu  ya Takukuru kamanda wa taasisi hiyo Wilaya ya Mbinga Frederick Msae amehudhuria mkutano huo kisha kutoa elimu shirikishi ya rushwa na kuwa itapelekwa kwenye kata za madiwani ili kutoa fursa kwa Wananchi wengi wakiwemo Viongozi kupatiwa elimu hiyo.



Diwani wa kata Kilimani Alex Andoya baada ya kutambua kuwa taasisi zingine zimetuma wawakilishi ambao hawana majibu sahihi kufuatia hoja za madiwani,diwani huyo amemshawishi mwenyekiti na baraza zima la Madiwani la kuwataka baraza la kikao kijacho taasisi hizo wafike Viongozi husika ili wajibu hoja kikamilifu jambo ambalo lilipokelewa kwa nguvu huku mwenyekiti Kelvin Mapunda akiwataka wawakilishi waliotumwa na mameneja wao wakafikishe salamu za kikao kijacho wanahitajika.


Mwenyekiti Mapunda amesema mara kadha taasisi hizo zimekuwa zikifanya mchezo huo wa kutuma wawakilishi jambo ambalo limekuwa likisababisha baadhi ya hoja kushindwa kupatiwa majibu sahihi ya utekelezaji wake.



Baadhi ya hoja kwa upande wa Tarura inadaiwa na madiwani huo kuwa kumekuwepo na maeneo ambayo barabara zake hazipitiki ,kwa upande wa umeme baadhi ya Vijiji havijapatiwa huduma hiyo licha ya nguzo kuwepo maeneo hayo kwa muda mrefu ,huku Mbiwasa wanadaiwa bado kumekuwepo na kero ya maji kwa baadhi ya maeneo ,ambapo hoja hizo zimekosa kupatiwa majibu kutokana na kutokuwepo kwa wakuu wa taasisi hizo.



Aidha katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amemuagiza mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Grace Quintene kuhakisha wanasimamia Sheria ya baadhi ya Wananchi kulima(Mshindi) mazao marefu ndani ya Mbinga mji jambo ambalo inadaiwa kuwa ni kinyume cha taratibu.


Kwa upande wake mkurugenzi huyo akipokea maagizo hayo amesema kuwa atayafanyia kazi na kuwa wale wote ambao watakuwa wamelima mazao hayo ndani ya Mbinga mjini watachukuliwa hatua.


    


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS