Header Ads Widget

TEMESA YAZITAKA TAASISI ZA UMMA WANAZOZIDAI BAADA YA KUPATIWA HUDUMA KULIPA MADENI

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


WAKALA wa Umeme na Ufundi Tanzania TEMESA umetoa wito kwa Taasisi za Umma zinazodaiwa na Wakala huo baada ya kupatiwa huduma za matengenezo ya magari, mitambo, huduma za ufundi, umeme na elektroniki, kuilipa TEMESA madeni inayowadai ili Wakala huo uweze utekeleza majukumu yake kwa ufanisi.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro. Kilahala metoawito huo Jijini DODOMA Wakati akizungumza katika kikao cha Wadau wanaopatiwa huduma na TEMESA Mkoa wa Dodoma, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ulioko Makole mjini Dodoma .


Kikao hicho kilihudhuriwa na maafisa mbalimbali wanaowakilisha Taasisi za Umma wakiwemo maafisa usafirishaji, maafisa kutoka Serikali kuu, Wizara mbalimbali, wawakilishi wa karakana teule zinazofanya kazi kwa pamoja na TEMESA na wazabuni wanaosambaza vipuri na vitendea kazi mbalimbali kwa Wakala huo


" Kulikuwa na malalamiko kwa baadhi ya wateja wanaotamani kulipa lakini Changamoto ilikuwa hawaelewi wanalipaje madeni hayo na ndio sababu ya kuwaweka hawa mabarozi ili kulahisusha zoezi hili," Amesema Kilahala



Akizungumza kuhusu madeni ambayo Wakala unadaiwa na wazabuni ambao waliikopesha vipuri miaka ya nyuma, Kilahala amesema TEMESA haipuuzii na wala haijasahau kama inadaiwa na wazabuni na kwamba  imekwishaundwa Timu kwa ajili ya kuyahakiki madeni hayo ikiwashirikisha wataalamu kutoka TEMESA.


"TEMESA haipuuzii na hauwezi kusahau Kama inadaiwa na wazabuni madeni yote yatalipwa hatuwezi kudhurumu kumbukeni hata Rais wetu was awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassani hapendi dhuruma anapenda hali, "anesema



Naye Meneja wa TEMESA Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Greyson Maleko, akizungumza katika kikao hicho, umehidi kuwa Wakala utaendelea kuwapatia huduma iliyo bora wakati wote na kwa ufanisi mkubwa ili na wao waweze kutekeleza majukumu yao kwa wakati na ufanisi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS