Header Ads Widget

"KUCHANGIA DAMU NI ZOEZI LA IMANI"_DEWJI

 




NA AMINA SAIDI_TANGA


Wakuu wa mikoa nchini wameombwa kuwekeza nguvu zao katika kukuza vipaji vya michezo kwa vijana ili kuweka timu ya wachezaji watakao wakilisha katika michezo ya kimataifa.


Hayo aliyasema  Azim Dewji ambaye ni WHO IS HUSSEIN FOUNDATION  na mfadhili wa timu za Coastal union na  African Sports iliyopo jijini Tanga ambazo zitacheza mechi ya kirafiki katika viwanja vya mkwakwani ikiwa uzinduzi wa taa za uwanja wa mpira wa mkwakwani kuelekea kilele cha miaka 46 ya CCM tarehe  5 February mwaka huu. 


Aidha alitoa ombi  hilo  wakati akiwaelezea waandishi wa Habari  kuhusu zoezi la uchangiaji  wa Damu ambalo limefanyika katika viwanja vya mkwakwani kwa lengo la kuokoa maisha ya watu ambao wana uhitaji wa Damu .


Aliongeza kusema zoezi la uchangiaji wa Damu ni zoezi la imani ambalo mtu hufanya kwa ajili ya kuokoa maisha ya mtu mwingine hivyo amewapongeza wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kwani tayari wameshakusanya uniti 450 ambapo wanatarajia  kuvuka lengo  mpaka mwisho wa zoezi.


 Sambamba na hayo aliwapongeza Azam kwa kufunga mataa kwenye viwanja vya mpira hususani mkwakwani  lakini pia itaweza kuwasaidia  washabiki  kutokuacha shughuli zao kwani wataangalia michezo usiku na kufika viwanjani wakati tayari wamemaliza shughuli zao.


Kwa upande wake mratibu wa Maabara ya mkoa wa  Tanga Juma Kayanda alisema kuwa mwitiko wa wanachi ni mkubwa wa kuchangia Damu kwa hiyari kiasi kwamba mpaka kufikia saa nane mchana tayari wamekusanya uniti 450 ambapo wanatarajia kuvuka lengo .


Aidha alisema mwitikio huo katika mkoa wa Tanga mwaka uliopita  walifikia asilimia 78 ambayo inaridhisha ambayo sasa inaokoa maisha ya watanzania.


"Kuna ajali iliyotokea huko Korogwe na kusababisha vifo na majeruhi  hivyo kwa mwitikio huo tayari majeruhi watapatiwa Damu kwani tuna Damu ya kutosha.,"alisema Kayanda.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS