Header Ads Widget

TAFU WANASIASA MUACHE KUFANYA UVUVI KAMA AJENDA YA KISIASA

 .














Chama cha Wavuvi Tanzania ( TAFU ) kimewaomba wanasiasa wote nchini kujiepusha  kufanya suala la uvuvi kuwa suala la kisiasa kutokana na baadhi ya wanasiasa kuanza kutoa lugha ambazo zinaweza kuchochea kufanya uvuvi ambao unaweza kuleta madhara ndani ya ziwa Victoria ikewemo uvuvi  haramu.


 


‘’ Hatuwezi kuepuka siasa na maisha yetu lakini tunaofika kwenye masuala ya kitaalamu wanasiasa watimize wajibu wao kwa kushauri tu, sisi kama wavuvi atuwezi kukubali ziwa Victoria ligeuke kuwa ajenda za uchaguzi mkuu wa Serikali  katika majukwaa ya kisiasa, Bakari Kadabi  - Mwenyekiti ChAma cha wavuvi  Tanzania, Tafu.


 


Mwenyekiti wa Chama cha wavuvi  Tanzania ( TAFU ) Bakari Kadabi  amewaomba wanasiasa nchini watusaidie kuelimisha baadhi ya wavuvi , maafisa uvuvi , watendaji wa vijiji, wenyeviti wa serikali na wengineo wote kuacha kujihusisha na uvuvi haramu, ili waache na watambue umuhimu wa kulinda raslimali za nchi kwa faida ya Watanzania wote.


 


“ Tunaiomba Serikali ihakikishe samaki analindwa kama wanavyolindwa wanyama pori katika hifadhi za taifa na inasikitisha kuona maliasili zote zinalindwa kwa kutumia nguvu kubwa sana kuliko maliasili ya uvuvi, Bakari Kadabi  - Mwenyekiti ChAma cha wavuvi  Tanzania, Tafu.


 


Chama cha wavuvi Tanzania kikiongozwa na mwenyekiti wake Bakari Kadabi wamekuwa msitari wa mbele katika kuhakikisha wanasimamia suala zima la kulinda rasilmali ya samaki ndani ya ziwa Victoria kutokana na uwepo wa kushamiri kwa vitendo vya uvuvi haramu katika ziwa hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS