Header Ads Widget

TASAF IFUNDISHE STADI ZA KUKUZA KIPATO - RC SENDIGA

 




Na. FRANCO NKYANDWALE MATUKIO DAIMA APP RUKWA.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga ameagiza wataalam wanaosimamia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika ngazi ya Halmashauri kuwafundisha wanufaika stadi za kazi zitakazosaidia kuinua kipato cha wananchi.


Ametoa kauli hiyo jana wakati kukagua kikundi cha wanufaika wa TASAF waliopo kijiji cha Ilemba Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wanaojishughulisha na mradi wa miti ya matunda na mbao.


“Wafundisheni wanufaika hawa kuwa na miradi yao ya mashamba ya miti au ufugaji mifugo katika kaya zao ili kipato kidogo wakipatacho toka serikalini kiwe ni mtaji wa kukuza uchumi . Wafikirie kubuni miradi siyo kutegemea fedha za TASAF” amesema Sendiga.


Sendiga aliongeza kwa kusema kuwa fedha wanazopata wanufaika siyo fungu la mirathi na kuwa wasipewe kama sadaka bali wafundishwe ujasiliamali wa kuwa na miradi yao ili siku serikali ikisitisha mipango hiyo waweze kujitegemea.


Nao wanufaika wa TASAF toka kijiji cha Ilemba waliozungumza na MATUKIO DAIMA walikuwa na haya ya kusema, Everada Kapaya alisema kuwa amenufaika na mfuko wa TASAFU tangu mwaka 2015 ambapo ameweza kujenga nyumba ya vyumba viwili na kusomesha watoto wake wanne pamoja na kuanzisha ufugaji wa ng’ombe mmoja .


Evarada alisema ‘nashukuru serikali kwa mradi huu wa TASAFU na ninaomba Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kutusaidia ili tuweze kusomesha watoto wapate elimu nzuri” .


Naye Elizabeth Pesambili mkazi wa Ilemba alisema kuwa kupitia mfuko wa TASAFU ameweza kulea wajukuu zake 16 ambao aliachiwa na watoto wake  na kuwa sasa ana miaka mitano akipata pesa toka serikalini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS