Header Ads Widget

SHIRIKA (NLF) LAJITOLEA KUGAWA VITI MWENDO BURE KWA WALEMAVU KILIMANJARO

 



Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP,_MOSHI


Watu wenye ulemavu hususan wanaohitaji viti mwendo ili kuweza kuwasogeza kutoka eneo moja hadi nyingine imeonekana kuwa ni changamoto kubwa inayowakabili hivi sasa.


Wakizungumza katika siku maalum ya watu wenye ulemavu(night to Shine)iliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la New Life Foundation (NLF)baadhi ya walemavu hasa wa uti wa mgongo walionekana kuhitaji uangalizi wa kina katika upatikanaji wa viti mwendo.


Aidan Shayo ambaye ni mlemavu wa uti wa mgongo amesema Kwa sasa ipo haja ya kuona namna ya kupata viti hivyo kwa gharama nafuu zaidi ili kuweza kuwasidia walio wengi.


'Wapo watu ambao ni walemavu lakini wanashindwa kununua vitu mwendo na hii inapelekea waendelee kubaki ndani kumbe wangeweza kutoka na kufanya shughuli ndogondogo zakuwaingizia kipato"alisema



Amesema kuwa kwa sasa serikali imeonekana kuwakumbuka watu wenye ulemavu tofauti na kipindi cha nyuma ambapo jamii hiyo ilionekana kusahaulika au kubaguliwa kwenye masuala mbalimbali.


Rose Kishia ambaye naye ni mlemavu aliyepooza miguu amesema suala la kukosekana kwa viti mwendo bado ni changamoto ambayo inahitaji kuangaliwa kwa jicho la kipekee.


"Sisi ambao tuna ulemavu ambao tunatumia hivi viti mwendo huwa tunakumbana na changamoto kubwa ya upatikanaji wake kwani vinauzwa bei ghali na hata ukiona wengi wanavyo basi ujue kuna mfadhili kajitokeza"anasema  



Rais wa NLF nchini Dkt Glorious Shoo amesema katika kutatua changamoto hiyo tayari amefanya mazungumzo na taasisi ya (EPT)

Epignosis physiotherapy Clinic ambao wanatengeneza viti hivyo na kuwa watagawa kwa walemavu wenye uhitaji kwa mkoa mzima wa Kilimanjaro


"Tayari tumeshafanya mazungumzo na EPT ambao wanatengeneza viti mwendo mwanzoni walitaka mlemavu achangie 50000 lakini gharama hizo sisi tutazibeba hivyo kwa mwenye uhitaji anaweza kufika ofisini ili kuweza kumuunganisha na hawa wataalam"amesema


Katika hatua nyingine Dkt Shoo amekemea vikali baadhi ya watu katika jamii kuwatumia watu wenye ulemavu kama sehemu ya kitega uchumi na kuwa hali hiyo haikubaliki na kuwa inaondoa utu wa mtu.



"Kuna mtu anawachukua hawa ndugu zetu alafu anawapa vibaiskeli na watu wakuwatembeza alafu jioni anawatoza fedha hivyo anajinufaisha kupitia wao"anasema


Dkt Shoo amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa watu hao (NLF)wakiandaa siku hiyo muhimu ikiwa ni jitihada za kuwatambua lakini pia kuwafariji kutokana na hali ya ulemavu waliyonayo


Alisema sherehe hiyo iliyokwenda sambamba na kuwatunuku vyeti ni faraja kwao lakini pia kuikumbusha jamii kuwa ulemavu unaweza kumpata mtu yoyote kwa wakati wowote ule hivyo kama jamii haina budi kutambua mchango wa watu wenye ulemavu waliopo kwenye jamii zetu.


"Haiwezekani mtu ni mlemavu anazungushwa tena kwenye jua Kwa kisingizio cha kuomba msaada lakini naomba kuikumbusha jamii kuwa suala la ulemavu ni suala la dakika moja tu hivyo ni lazima kama jamii sasa tuone umuhimu wa hawa wapendwa wetu"alisema


Shedrack Domingo nimkurugenzi wa (EPT) Epignosis physiotherapy Clinic ambapo amesema tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka 2020 zaidi ya viti 170 vimeshagawiwa kwa wenye uhitaji


Amesema katika utengenezaji wa viti hivyo wamekuwa wakitumia vipuri ambavyo vinapatikana kirahisi kwa fundi baiskeli mitaani tofauti na vile ambavyo vinaagizwa toka nje ya nchi ambapo ukarabati wake ni mgumu kutokana na malighafi zulizotumika kutengeneza.


"Vile vya kutoka nje vimetengenezwa mahususi kwa mazingira ya barabara za kwao maana zina lami tofauti na huku kwetu ambapo havichukui muda mrefu bila kuharibika"alisema



Amesema kwa kushirikiana na NLF sasa wataweza kutengeneza viti hivyo ambavyo vitawafikia walio wengi na kuwa vipimo vyote na viwango vinavyotumika vimethibitishwa na shirika la afya duniani(WHO).


Alisema kinachohitajika ili mhusika aweze kukipata na kuwasiliana na NLF ambapo wait watawasiliana na sisi kisha tumfuate mteja alipo na tumpime uzito na upana kabla hatujaanza kutengeneza jambo ambalo ni tofauti na vinavyotoka nje.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI