Header Ads Widget

WAKAZI WA KIJIJI CHA MHEKELA NA KITELEA WILAYA YA MBINGA WAMEISHUKURU SERIKALI KWA KUSAIDIA UJENZI WA ZAHANATI KWENYE VIJIJI HIVYO

 


 Amon Mtega,Mbinga

WAKAZI wa  Kijiji cha Mhekela na Kitelea vilivyopo kata ya Kilimani Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Wakazi hao katika Ujenzi wa Zahanati kwenye vijiji hivyo.


Akizungumza mwenyekiti wa Kijiji cha Mhekela Samwel Mbele amesema kuwa Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho uliibuliwa na Wananchi na kisha Serikali kupitia diwani wa kata hiyo Alex Andoya na Halmashauri ya Mbinga mji wamechangia ujenzi huo ambao bado unaendelea kukamilika .


  Kwa upande wake mtendaji wa Kijiji hicho Francis Kiyagi amesema mradi wa Zahanati hiyo unatarajia kukamilika Marchi mwaka huu na kuwa kiasi cha shilingi milioni 98 zinatarajiwa kutumika ambapo Halmashauri ya Mbinga mji imeshatoa shilingi Milioni 45 fedha nyingine za kukamilisha mradi huo zinatolewa na Wananchi kufuatia  makubaliano ya pamoja .



   Naye mkazi wa Kijiji cha Kitelea Ponsia Mbunda ambapo Zahanati yao imekamilika kwa asilimia karibu 90 amesema kuwa uwepo wa Zahanati hiyo utawapunguzia adhaa waliyokuwa wakikutana nayo ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu.


Mwananchi Mbunda amesema kuwa waliokuwa wakipata shida zaidi ni wanamama wajawazito jambo ambalo limekuwa likiwapeleka baadhi yao kujifungulia njiani na kuhatarisha maisha ya mama na mtoto.



 Kwa upande wake diwani wa kata ya Kilimani Alex Andoya amesema kuwa kata hiyo inavijiji saba na katika vijiji hivyo vitatu ndivyo vyenye Zahanati mkakati ni kuhakisha Vijiji vyote vinapatiwa Zahanati ili kupunguza adhaa zilizokuwa zinawakabili Wananchi.


 Diwani Andoyo amevitaja vijiji ambavyo tayari Zahanati zake zinatumika kuwa ni Kilimani,Sepukila na Mkwaya ambapo mkwaya Wananchi wake wanatumia Zahanati ya magereza na kuwa mikakati ya Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji katika eneo hilo unaendelea.


Aidha diwani huyo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga mji Grace Quintene ikiwemo na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda kwa kazi mbalimbali zinazofanyika kwa Wananchi ikiwemo kuwakamilishia miradi kama ya Zahanati.


    

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI