Header Ads Widget

"RAIS DKT SAMIA ANA MAONO YA MBALI"_UVCCM

 



Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP MOSHI.


Imeelezwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi wa kipekee ambaye anajali makundi yote katika jamii bila kubagua jambo linalozidi kuongeza ustawi na mshikamano kwa taifa.


Hii imetokana na utaratibu ambao amekuwa akiufanya kwa kukutana na makundi mbali mbali ambapo mwishowe kumekuwa kukipatikana matokeo chanya kwa pande zote yaani serikali na wananchi.


Februari 11, 2023 Ikulu jijini Dodoma, Rais Samia alikutana na viongozi wa Tahliso na Zahlife kwa upande wa Zanzibar ambapo aliwapa nafasi ya kuuliza maswali na kuzungumza nao kuhusu mambo mbalimbali yanayowahusu.




Katika mkutano huo, Rais wa Tahliso, Frank Nkinda amewasilisha maombi yao kwa Rais Samia ili aweze kuwasaidia wanafunzi hapa nchini kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha.


Moja ya maombi yaliyowasilishwa na Nkinda ni pamoja na kuongezewa kiasi cha fedha za kujikimu kinachotolewa na serikali kwa wanafunzi kwa siku kutoka Sh8,500 za sasa hadi kufikia Sh10,000 kwa sababu maisha yamepanda.




Rais Samia Suluhu Hassan aliridhia ombi la viongozi wa shirikisho la wanafunzi wa Ttaasisi za elimu ya juu Tanzania (Tahliso) la kutaka kuongezewa fedha za kujikimu kutoka Sh8,500 kwa siku hadi Sh10,000.




Yuvenail Shirima ni mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini ambapo alisema jambo hilo linaenda kuleta faraja kubwa kwa wasomi hao sambamba na kuwapunguzia ukali wa maisha.




"Sisi UVCCM ndio walezi wa seneti hivyo hawa wanapopata tatizo huleta kwetu kama walezi wao na sisi tunalifikisha sehemu husika jambo la kushukuru ni kuwa yamefanyiwa kazi"anasema 




Katika hatua nyingine Shirima alisema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye maono ya mbali kutokana na kukutana na makundi mbali mbali na kuzungumza nao kwa lengo la kuwasikiliza na kuwapatia suluhisho.




"Alishakutana na viongozi wa vyama vya siasa hatimaye mikutano ikaruhusiwa sasa kakutana na hawa wasomi 'boom'limeongezwa hivyo unaona ni jinsi gani amekuwa kiongozi wa kushirikishana na wengine"anasema 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI