Header Ads Widget

RC CHALAMILA AWAONYA WAZAZI WANAOWAOZESHA WANAFUNZI

 



NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.


MKUU wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila, amewaonya wazazi wanaoozeesha watoto wao kwa kisingizio cha kutokuwa na hela ya kununua mahitaji madogo madogo ya kujiunga kidato cha kwanza.


Hayo ameyasema katika uzinguzi wa shule ya sekondari Kitobo iliyoghalimu zaidi ya shilingi Mil.400, iliyoko kijiji cha Kitobo kata kitobo wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, ambapo amesema kuwa serikali imetumia pesa nyingi kujenga vyumba vya madarasa ili kutatua kero waliokuwa wakikumbana nayo kipindi cha nyuma  ya uhaba wa madarasa, hivyo hatafumbia macho wazazi pamoja na viongozi ambao watakaonekana kushirikiana  kuwakozesha watoto kwa sababu zotote zile kama vile kisingizio cha kukoswa pesa, kuwaozesha na wengine kuwapleka watoto wao kufanya kazi za ndani.


"Juzi niilitoa agizo la kukamatwa diwani wa Ibwera aliyeshirikiana na wazazi kumuozesha mtoto ambaye alitakiwa kujiunga kidato cha kwanza na hivi tunavyoongea leo zaidi ya wazazi kumi na moja wameishakamatwa na kuwekwa ndani kwa sababu hii hii ya kuozesha watoto wao ambao walitakiwa kuwa shule, niseme ukweli ya suala hii nimelivalia njuga sitamuonea haya mzazi wala kiongozi yeyote atakayebainika kumuozesha mtoto wake"


Aidha amewahisi wanafunzi katika shule hiyo kusoma kwa bidii ili waweze  kuwasaidia wazazi wao pamoja na jamii yao kwa ujumla huku akiwaonya kuepuka kujihusisha na vitengo viovu hasa mahusiano kwani itapelekea kushindwa kutimiza malengo yao.


Sambamba na hilo mkuu wa mkoa huyo  amewasihi wahitimu wa vyuo vikuu nchini kutokukata tamaa na kutumia elimu na maarifa waliyoyapata kutafuta namna ya kujipatia kipato sio kusubiri ajira za serikali tu huku akiwasihi wazazi pamoja na wahitimu hao kuacha tabia za kuilahumu serikali kuhusu ajira kwani serikali ya awamu ya sita imeajiri na inaendelea kuajiri watumishi katoka kada mabalimbali Kadri iwezavyo.



Aidha mwenyekiti wa kijiji George Kassano, Kitobo wakati akitoa neno lake mbele ya mkuu wa mkoa, ameipongeza serikali hasa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suruhu Hassan kwa kusikia kilio chao cha uhitaji wa  shule kwani shule hiyo itawasaidia kuondoa kero ya watoto wao kutembea  mwendo mrefu zaidi ya kilometa 10  kuifuata  shule ya sekondari Bwabuki iliyopo kijiji jirani.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS