Header Ads Widget

BARAZA LA TAIFA LA UJENZI LIMEENDESHA MAFUNZO KWA WADAU 155 BARA NA VISIWANI

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


BARAZA la Taifa la ujenzi limeendesha mafunzo ya kusimamia mikataba ya ujenzi na utatuzi wa migogoro katika miradi ya ujenzi kwa wadau 155 kutoka Tanzania bara na Tanzania visiwani.


Mtendaji Mkuu wa baraza la taifa la ujenzi Dkt,Matiko Mturi Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa  baraza hilo katika serikali ya awamu ya sita.


Dkt Mturi amesema wameandaa Rasimu ya Mapendekezo ya gharama za msingi za ujenzi wa barabara (base unit rates) kwa kila mkoa wa Tanzania bara na kuwakilisha katika kikao cha wadau wa ndani ya serikali ili kupata maoni na ushauri wao.


Aidha amesema wanaendelea kuratibu utatuzi wa migogoro ya miradi ya ujenzi kwa njia ya adjudication na arbitration ambapo jumla ya mashauri 6 yametolewa uamuzi na 31 yanaendelea katika hatua mbalimbali za utatuzi.


" Baraza limefanikiwa kuratibu ,kuandaa na kuwasilisha Wizara ya ujenzi na uchukuzi(sekta ya ujenzi) andiko dhana (concept note) lenye mapendekezo ya kuboreshwa kwa mfumo wa sheria zinazosimamia ujenzi wa nyumba na majengo nchini,"Amesema Dkt MturiH


Hatahivyo mipango ya utekelezaji kwa  februari 01 2023 hadi Juni 30 2023 kukamilisha kuandaa mapendekezo ya gharama za msingi za ujenzi wa barabara kwa kila mkoa wa Tanzania bara na kupata maoni na ushauri wa wadau nje ya serikali hususani wakandarasi na washauri elekezi.


“Tunatoa mafunzo ya kusimamia mikataba ya ujenzi na utatuzi wa migogoro katika miradi ya ujenzi kwa wadau wa sekta ya ujenzi hususani taasisi za umma zinazotekeleza miradi ya miundombinu”Amesisitiza Dkt Mturi


Dkt Mturi amesema mwelekeo wa taasisi katika kutekeleza majukumu ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa sera ya ujenzi nchini,kuandaa na kutekeleza mpango mkakati wa maendeleo wa sekta ya ujenzi,kutoa miongozo mbalimbali ya kitaalam ya maeneo mbalimbali ya ujenzi.


Ameeleza kuwa kuanzisha wiki ya huduma ya sekta ya ujenzi kwa wakati mmoja na kongamano la wadau wa ujenzi kwa lengo la kuimarisha uhusiano,ushirikiano hivyo kuongeza ubunifu na tecknolojia miongoni mwa wadau katika sekta hiyo


"Taasisi itaendeleza  kutoa mafunzo kwa wadau wa ujenzi kuhusu maadili na utekelezaji wa miradi ya ujenzi, sanifu_jenga na usimamizi wa mikataba ya ujenzi kwa wadau mbalimbali pamoja na kutoa mafunzo yanayolenga kukuza na kujenga wataalam mahiri katika sekta ya ujenzi, " Amesema Dkt Mturi

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI