Na Gift Mongi, MATUKIO DAIMA APP MOSHI.
Mwenyekiti UVCCM wilaya moshi Vijijini, Yuvenail Shirima, ameahidi kutatua kero mbali mbali zinazowakabili vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi sanjari na kufanya shughuli za kimaendeleo.
Akiongea katika mkutano wa hadhara alioufanya wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)tawi la mikocheni kata ya Arusha chini alisema changamoto kadhaa zinazowakabili vijana hao ataenda kuzitafutia suluhisho.
Aidha kwenye mkutano huo Shirima alisikiliza kero za vijana kama upatikanaji wa mikopo kwa vijana, upatikanaji wa viwanja vya michezo, vifaa vya michezo, kadi za UVCCM na CCM .
"Niwahakikishie tu kuwa zipo kero nyingine ambazo sitaweza kuzitolea majibu ya moja kwa moja hapa ila nawahakikishia kuwa nitaenda kuja na majibu siku sio nyingi"amesema
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo aliwasisitiza vijana kuwa wabunifu sanjari na kuchangamkia fursa za mikopo isiyo na riba inayotolewa na halmashauri.
Alisema fedha zile ni mahususi Kwa ajili ya vijana wanawake na watu wenye ulemavu na kuwa vijana wakijiunga na kuhamua kuwa wabunifu zinaweza kuwainua kiuchumi.
"Naomba kuwaahidi kuwa nitapambana hadi dakika ya mwisho kuhakikisha fedha hizi na nyie mnaenda kunufaika nazo na sio ziende kwa wengine na wengine wakose hii hapana"alisema
Shirima ambaye pia ni mdau wa michezo alichangia mipira miwili ya mchezo wa miguu na alipata wasaa wa kuendesha harambee iliyofanikisha kukusanya kiasi cha shilingi 470,000 ambapo 250,000 zitatumika kununua nyavu kwa ajili ya magoli ya mpira wa miguu na 220,000 kutumika katika kufungua akauti ya vijana wa tawi la Mikocheni kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya vijana.
Nicholous Mdeme ni miongoni mwa vijana waliohudhuria kwenye mkutano huo ambao alisema imekuwa ni faraja kwao kukutana na vijana ambapo pia inawasaidia kubadilishana uzoefu na changamoto mbalimbali.
"Nashukuru tunavyokutana hivi huwa tunabadilishana uzoefu lakini kuona jinsi ya kupata suluhisho na niwahamasishe vijana wawe wanajitokeza pindi wanaposikia kuna mikutano"amesema
0 Comments