Header Ads Widget

"MARUFUKU KUUZA ,KUTENGENEZA MAJENEZA KANDOKANDO YA HOSPITALI" RC BABU

 


Na Gift Mongi,MATUKIO DAIMA APP, MOSHI


Watengenezaji na wauzaji wa majeneza kwenye maeneo ya hospitali mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuondoka mara moja katika maeneo hayo.


Agizo hilo la serikali limetolewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu ambapo amewaagiza wakuu wa wilaya kusimamia zoezi hilo na wahusika wakatafute maeneo mengine yakuendeahea shughuli zao.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Babu amesema biashara hiyo ni lazima kufanyika kwa kufuata utaratibu mzuri na kwa kuwa ni lazima yatengenezwe na kuuzwa ni vyema ukawepo utaratibu ikiwa ni pamoja na kuwa na maeneo yao.


"Majeneza ni lazima yatengenezwe na kuuzwa ila naagiza wakuu wa wilaya wote wahakikishe wanawaondoa hawa wauza majeneza na wawe na maeneo yao kama walivyo kwa mafundi seremala"amesema


Alisema wanaofanya biashara hiyo ndani ya hospitali au nje waondoke na kama itatokea mtu amefariki ndugu wa marehemu wataenda kutafuta jeneza huko litakapokuwa linapatikana Kwa wakati huo na sio maeneo ya hospitalini


"Tunapowachia hawa wakaendelea kuuza na kutengeneza kandokando ya hospitali ni kama tunataka watu wafe ila hapa Kilimanjaro hawatakufa"amesema Babu


Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa ni kuwa mgonjwa anapoenda hospitali anakuwa na matumaini ya kupona ugonjwa wake lakini pindi anapoona majeneza huanza kukata tamaa ya kuishi na sio matamanio ya hospitali kuona mgonjwa alipoteza maisha.


Lucas Gondwe ni mkurugenzi mwenza wa kampuni ya huduma za mazishi ya  GodMark ya mjini Moshi ambapo amesema kuuza au kutengeneza majeneza kandokando ya hospitali ni sawa na kuomba wagonjwa wafariki ili biashara ifanyike


Amesema wao kama watengenezaji wa majeneza walihamua kujitenga na kukaa mbali na hospitali kwa kuwa mgonjwa anapopelekwa hospitali akiona jeneza huanza kuingiwa na woga na kuanza kubadili fikra


"Hospitali ni sehemu ya faraja lakini sasa mtu anapoenda kutengeneza majeneza pale mlangoni ni sawa na kuwaambia wagonjwa mkiingia hamtarudi salama kitu ambacho sio kweli"alisema


Amesema hata kama wamehamua kufanya biashara hiyo itumike njia sahihi katika kuyahifadhi ili yasionekane kirahisi na pindi mtu atakapokuwa anahitaji ndipo aoneshwe na sii kuweka hadharani kama ilivyo kwa sasa.


Amesema kwa kuwa majeneza ni huduma yakitengenezwa nje au mbali ya hospitali ndugu wa marehemu wataweza kufuata pindi itakapohitajika.


"Mbona pale stendi hakuna mafundi gari ila ikitokea gari limeharibika basi mwenye gari atafuata gereji ilipo ni sawa na mtu akihitaji jeneza basi atalifuata huko litakapokuwa linapatikana"amesema Gondwe




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI