Header Ads Widget

SAKATA LA BIASHARA YA MAGENDO YA VILEO LACHUKUA SURA MPYA

 



NA MWANDISHI WETU - MATUKIO DAIMA


SAKATA la biashara ya magendo ya vileo Zanzibar limechukua sura mpya baada ya CCM Zanzibar kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua dhidi ya kampuni zinazojihusisha na magendo na kusababisha serikali kupoteza mapato.


Hayo yameelezwa na Katibu wa Idara ya itikadi na uenezi na habari, Khamis Mbeto Khamis alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya chama hicho Kisiwandui, baada ya kampuni ya MGW2014 Enterprises kutuhumiwa kuingiza vileo vya magendo alfajiri ya Febuari 12 mwaka huu.


Mbeto, amesema serikali ya awamu ya nane imekusudia kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake na biashara ya magendo inapaswa kupiigwa vita na vyombo vya ulinzi na mamlaka za kukusanya kodi Zanzibar.


Amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kusimamia ipasavyo sheria hasa katika kupambana na mianya ya ukwepaji wa kodi kwak uhakikisha taratibu za kisheria zinazingatiwa.


mjadala mkubwa umeibuka kwa wanasiasa, wanaharakati na mamlaka za ukusanyaji wa kodi baada ya Kampuni ya MGW2014 Enterprises kutuhumiwa kuingiza vileo kwa njia ya magendo Febuari 12 mwaka huu licha ya msimamizi wa kampuni hiyo Ali Seif kukanusha kampuni yake kujihusisha na magendo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI