Header Ads Widget

MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA MBINGA JOSEPH MDAKA AMEWATAKA WANACCM NA WANANCHI KUENDELEA KUKIAMINI CHAMA HICHO.

 

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbinga Joseph Mdaka akipanda  mti katika siku ya maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama hicho.

Na Amon Mtega,Matukio Daima,

         Mbinga.

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Joseph Mdaka amewataka Wananchi wa Wilaya hiyo kuendelea kukiamini chama cha CCM na Serikali yao inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili izidi kuwaletea maendeleo.


 Wito ameutoa wakati maadhimisho ya miaka 46  ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM ambapo maadhimisho hayo kiwilaya yamefanyika Kata ya Langiro Wilayani humo.


Mwenyekiti huyo akizungumza na Wananchi waliyojitokeza kwenye maadhimisho hayo amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa CCM na kushika dola mambo mbalimbali yakimaendeleo kwa Wananchi yamefanyika hivyo ni vema Wananchi wakaendelea kukiamini chama na Serikali.


Mdaka  licha ya kuwataka Wananchi wakaendelea kukiamini chama cha CCM na Serikali lakini bado amewataka wanaccm na wale ambao wanajiunga na Chama hicho kujisajili kadi zao za chama kwenye mfumo wa kisasa ili kutunza kumbukumbu zao kwa njia ya kisasa.


Aidha mwenyekiti huyo awali kabla ya mkutano huo amepita kukagua shughuli mbalimbali za utekelezaji wa ilani kisha kupanda miti ambapo amekagua ujenzi wa Bweni la Shule ya Sekondari ya Langiro, Ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Langiro pamoja na ujenzi wa Zahanati katika kata hiyo.



 Kwa upande wake katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mbinga Angelo Madundo akisoma taarifa ya Chama ya Wilaya kwa niaba ya katibu wa CCM Wilaya hiyo Mary Mwenisongole amesema kuwa Chama kinaendelea kushirikiana na watendaji wa Serikali kikamilifu katika kutekeleza miradi mbalimbali kwa Wananchi.


Madundo Akizungumzia suala la uchumi katika Wilaya hiyo amesema Chama kinaendelea kujipanga ikiwemo ujenzi wa vibanda vya biashara kuzunguka uwanja wa CCM,na ujenzi wa ofisi mpya ambao unaendelea kukamilika huku akisema uhai wa Chama wa kuwasajili wanachama kwa mfumo wa kisasa zoezi hilo kinaendelea.


Katibu huyo akizungumzia  kuhusu ushirikiano wa wabunge na madiwani katika utekelezaji wa ilani kwenye kukijenga chama amesema ni ushirikiano mzuri ambao unaonyeshwa na wachaguliwa hao ambapo katika Jimbo la Mbinga mji Mbunge wake ni Jonas Mbunda huku Mbinga Vijijini Mbunge wake ni Benaya Kapinga.


Aidha katibu Madundo baada ya taarifa hiyo ametumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa wanachama wa CCM na Wananchi kwa ujumla kuwa katika 46 ya kuzaliwa kwa Chama hicho kinakumbusha historia ambapo  kilizaliwa Februari tano mwaka 1977 siku ya Jumapili saa 10 katika uwanja wa Amani Zanzibar .


Amefafanua kuwa historia hiyo inawafanya wanaccm kuendelea kuimalika katika nyanja mbalimbali ikiwemo ibara ya tano ya kwenye katiba ya CCM ya 1977 kuhakisha kushinda chaguzi na kushika dola ambapo kwa sasa siku za hivi karibuni kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za mitaa na Vijiji lengo ni moja kushika dola chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.


 Maadhimisho hayo yamehudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na Viongozi wa dini mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuimalisha ushirikiano katika kutekeleza mambo ya jamii.

    








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS