Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa rai kwa Balozi za Tanzania nje ya nchi ziwasilishe takwimu za walimu wanaohitajika Kufundisha lugha ya Kiswahili katika nchi wanazowakilisha.
Mhe. Balozi Dkt. Chana ametoa rai hiyo Februari 22, 2023 alipofanya ziara ya kwanza katika Ofisi za Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) tangu alipoteuliwa na Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameilekeza BAKITA iendelee kuwa na matukio mengi ikiwemo makongamano, warsha mikutano na majukwaa mbalimbali ya kuendeleza na kubidhaisha lugha ya kiswahili ndani na nje ya nchi.
Nampongeza sana Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutumia lugha ya Kiswahili katika mikutano ya Kimataifa ikiwemo ya Umoja wa Afrika na Afrika Mashariki, pamoja na kuongeza Bajeti katika kubidhaisha lugha hii adhimu" amesema Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana
Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana amelielekeza BAKITA ishirikiane na Vyuo Vikuu vyenye vitivo vya lugha ya Kiswahili katika kuandaa Wataalamu wa lugha hiyo ili kuongeza ufundishaji wa lugha hiyo kwa ufasaha .
Awali, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Pauline Gekul akizungumza wakati wa kumkaribisha Waziri Pindi Chana, amelipongeza Baraza hilo kwa kuendelea kutekeleza vyema Mkakati wa wa miaka kumi wa kubidhaisha Kiswahili ulioanza mwaka 2022 hadi 2032.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bibi. Consolatha Mushi amesema Baraza hilo pamoja na mafanikio yaliyopo limefanikiwa kuadhimisha siku ya Kiswahili Duniani mwaka 2022 pamoja na kuandaa Mkutano Mkuu wa Idhaa za Kiswahili Duniani uliofanyika mwaka 2022 jijini Arusha.
0 Comments