Header Ads Widget

TTB YAAGIZWA KWENDA KIMATAIFA, KIDIGITI KUITANGAZA TANZANIA.



Katika mwendelezo wa kujifunza na kujipanga, leo Mhe Waziri Mohamed Mchengerwa, Waziri wa Maliasili na Utalii na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, wametembelea Bodi ya Utalii (TTB) jijini Dar es Salaam; chombo muhimu kilichopewa dhamana na dhima ya kutangaza na kufanya uraghibishaji wa sekta ya utalii ndani na nje ya nchi. 


“Hapa lazima tukiri yapo yaliyofanyika lakini bado tuna kazi kubwa kuutangaza utalii wetu ndani na nje ya nchi. Kazi ipo hapa. Nataka mje na mikakati zaidi na hasa kutumia teknolojia lakini pia tuwe na slogan moja inayoeleweka kuliko sasa kila mtu ana yake ili kuutangaza utalii kimataifa zaidi,” alisema Mhe. Mchengerwa.



“Mnaweza kuwa mmefanya mengi lakini Watanzania bado hawajaona kama mmefika pakubwa sana.Tuendako tutalala pamoja hapa kuja na mikakati kabambe kuendeleza pale Mhe Rais Mama Samia alipoishia katika Royal Tour,” aliongeza Dkt. Abbasi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI