Na THABIT MADAI- ZANZIBAR, MATUKIO DAIMA APP
CHAMA cha Mapinduzi Zanzibar, kimesema mafanikio makubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo yanaendelea kuonekana katika sekta ya elimu, miundombinu pamoja na uimarishaji wa huduma za maji visiwani Zanzibar.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Idara ya itikadi na uenezi na habari, Khamis Mbeto Khamis wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya chama hicho Kisiwandui kuhusu miradi ya ujenzi inayoendelea ikiwemo Soko la Mwanakwerekwe, Jumbi na Mbuzini.
Amesema ujenzi wa masoko hayo unatarajiwa kukamilika na kuzinduliwa januria mwakni lakini amesema serikali imeshaamua kulivunja soko la mbogamboga la Mombasa kwa mchina na kujenga soko la kisasa ambapo mradi huo utakamilika baada ya miezi minane.
Akizungumzia tatizo la mfumko wa bei, alisema kwamba hali hiyo ilisababishwa na ukame uliojitokeza katika mikoa ya Tanzania bara pamoja na mtikisiko wa kiuchumi uliojitokeza duniani baada ya kuibuka kwa marazi ya UVIKO-19 na vita vinavyoendelea vya Urusi.
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi, ameibua mjadala mmkubwa Zanzibar kutokana na miradi ya mkakati inayoendelea kujitokeza ikiwemo miradi ya nishati, miundombinu ya barabara, sekta ya elimu na kuimsrisha maslahi ya walimu tangu kushika wadhifa huo.
0 Comments