Wahitimu kidato cha sita mwaka 1992 Sekondari ya Loleza ya mkoani Mbeya watoa msaada kwa yatima na wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Morogoro.
Wanafunzi hao waliomaliza kidato cha shule ya Sekondari ya Loleza iliyopo mkoani Mbeya mwaka 1992 kupitia kikundi chao cha LOLEZA GIRL’S wamekutanika mkoani Morogoro na kwenda kutoa msaada kwenye kituo cha Kulelea Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Uzima Group Home kilichopo Mkambalani mkoani Morogoro.
Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi hicho kinachoundwa na watu zaidi ya 50 Asha Abdallah alisema lengo la kwenda kituoni hapo ni kuwafariji Watoto hao na kuwapa msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni michango yao wenyewe.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi hicho Zawadi Mwenda ametaja vifaa vya mahitaji ya misaada waliyotoa kuwa ni pamoja na unga wa mahindi, mafuta ya kupikia, Sabuni, sukari na kukabidhi kwa msimamizi wa Kituo cha Uzima Group Home Samuel Mashita ambaye alishukuru wahitimu hao kwa Msaada huo.
Katika hatua nyingine kikundi hicho kimekutana na Mwalimu wao Siangicha Mosha ambaye alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule wakati wakisoma ambaye pia walimpa zawadi mbalimbali kama Shukrani kwa msingi wa kuwafikisha katika hatua mbalimbali za mafanikio ya maisha yao.
Mstaafu huyo Mwalimu Siangicha alimshukuru Mungu kwa kuona mafanikio ya Vijana wake aliowalea na kuwafundisha pamoja na kuwashukuru wahitimu hao kwa Msaada waliompatia.
0 Comments