Header Ads Widget

JAMII YATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANASAYANSI WANAWAKE NA WASICHANA

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


JAMII imetakiwa kuunga mkono Juhudi za wanasayansi wanawake na wasichana katika kuimarisha mchango wa utafiti na ubunifu wa kisayansi wenye tija kwa ustawi wa uchumi kwa maisha ya kizazi cha leo na kesho.


Pia wadau wa sekta za umma na binafsi nao wametakiwa kuendelea kuunga mkono Juhudi hizo ili kuwezesha kukua kwa sekta zingine ikiwamo viwanda na sekta nyingine za kipaumbele ifikapo mwaka 2025


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi Omary Kipanga amesema jijini Dodoma wakati wa hafla la ya maadhimisho ya Kimataifa ya siku ya wanawake na Wasichana Katika sayansi ambapo amesema ubunifu unaofanywa na wanawake na wasichana unahitajika na unachangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi kwa taifa.



Ameeleza uwekezaji unaofanywa na serikali ya awamu ya sita katika miundombinu na rasilimaliwatu unasaidia kufanyika kwa utafiti wa kisayansi unaolenga kuzalisha bunifu na teknojia zinazojibu changamoto za watanzania.


"Maadhimisho hayo yanatumika kama sehemu ya kuwahamasisha wasichana na wanawake kuhamasika kusoma masomo ya sayansi, hisabati,uhandisi na ubunifu ili kuongeza namba za wanawake na wasichana katika soko la ajira kwa upande wa Sayansi," amesema.


Nakuogeza "Siku hii itumike kuwahamasisha wanawake na wasichana kujikita zaidi kusoma masomo ya sayansi, uandisi,hesabu,ubunifu na teknolojia,"amesisitiza Kipanga," Amesema Kipanga



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, teknolojia na ubunifu Prof.Maulilio Kipanyula amesema kuwa, nchi za Afrika ushiriki wa wanawake na wasichana katika masomo ya Sayansi, teknolojia,ubunifu na Hisabati ni asilimia 24 tu,hivyo maadhimisho hayo ni sehemu ya kuwahamasisha wanawake na wasichana kushiriki kikamilifu katika masomo ya Sayansi, teknolojia na ubunifu.


"Maadhimisho haya yanatumika kuhamasisha wanawake na wasichana kushiriki kikamilifu katika masomo ya sayasi,teknolojia,ubunifu na hisabati naamini tukifanya hivi hata huko kwenye soko la ajira wataongezeka,"amesema Kipanyula



Naye  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya afya na masuala ya UKIMWI Stanslaus Nyongo (Mb) amesema pamoja na jitihada kubwa za kuwasaidia watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi, bado kuna changamoto ya walimu wa masomo ya sayansi ni wachache.


"Jitihada ni kubwa sana zinazofanywa na Serikali ila bado kuna changamoto kwa upande wa walimu wanaofundisha masomo ya sayansi hivyo ni vyema tukaongeza jitihada katika kuwatengeneza walimu watakaokuja kuwa msaada katika kuwafundisha watoto hawa katika masomo haya ya Sayasi,hesabu,uandisi,na ubunifu,"amesema Nyongo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI