Header Ads Widget

KATIBU WA CCM WILAYA YA MBINGA AWATAKA WANACCM KUWA MFANO KWENYE USAFI WA MAZINGIRA.

 



Na Amon Mtega, Mbinga.



KATIBU wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Mary Mwenisongole amewataka wanaccm Wilayani humo kuwa mstali wa mbele kwenye usafi wa mazingira ili jamii iweze kujifunza umuhimu wa kufanya usafi kwenye mazingira yao wanayoishi na wanayofanyia kazi na hatimaye kuzuia magonjwa ya milipuko yanayotokana na uchafu wa mazingira.


Mwenisongole amesema hayo wakati akiongoza zoezi la ufanyaji usafi kwenye mazingira mbalimbali ya ofisi ya CCM ikiwemo na mazingira ya eneo inapojengwa ofisi mpya ya Chama hicho ngazi ya Wilaya.


 Katibu huyo akiwa na wajumbe mbalimbali wa CCM Wilayani humo amesema kuwa Chama hicho ndicho kilichoshika dola inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa hivyo ni vema wanaccm wakawa mfano wa ufanyaji kazi kwenye jamii ikiwemo usafi wa mazingira.



 Amefafanua kuwa kama wanaccm watakuwa mstali wa mbele katika suala nzima la usafi wa mazingira yanayowazunguka basi jamii nzima itaiga mfano huo na kuyafanya mazingira kuwa masafi siku zote jambo ambalo litasaidia kuendelea kutokuwepo kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindukindu ambapo Wilayani humo hakipo .


          

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI