Header Ads Widget

WANNE WAFARIKI BAADA YA HELIKOPTA KUGONGANA

  

 Watu wanne wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa nchini Australia baada ya Helikopta mbili kugongana zikiwa hewani.


Taarifa zinaeleza kuwa jumla ya watu 13 walikuwemo ndani ya Helikopta hizo, kati yao wanne wamefariki na watatu wako mahututi. 


Uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo bado unaendelea huku matokeo ya awali yakionyesha kuwa moja ya Helikopta hizo ilikuwa imeanza kupaa huku nyingine ikikaribia kutua ndipo zilipogongana.


Tukio hili limetokea katika mji wa Gold Coast uliopo katika Jimbo la Queensland, sehemu ambayo ni maarufu kwa watalii.   

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS