Header Ads Widget

UVCCM WILAYA YA ILALA WASHIRIKI SHUGHULI YA UJENZI LIWITI SEKONDARI






Umoja wa Vijana Wilaya ya Ilala ukiongozwa na Mwenyekiti wake ndugu Juma Mizungu umeadhimisha mika 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi kwa kufanya shughuli ya kijamii ya Ujenzi katika Shule ya Sekondari Liwiti, Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Alhaj Said Sultan Side.

Shule ya Sekondari Liwiti ni miongoni mwa Shule za Sekondari zinajengwa kwa Ghorofa katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Wilaya ya Ilala, Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amelekeza kiasi cha shilingi Bilioni 3 kwaajili ya ujenzi wa majengo mawili ya Ghorofa katika katika Shule ya Sekondari Liwiti.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Alhaj Said Sultan Side ameipongeza Jumuiya ya Vijana Wilaya ya Ilala kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuboresha Jumuiya hiyo lakini pia kwa kuamua kasmdhimisha Miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi kwa kushiriki Shughuli ya Ujenzi.

"Hongereni sana umoja wa Vijana Wilaya mnafanya kazi nzuri dana katika Wilaya yetu lakini pia hongereni kwa kuamua kushiriki shughuli hii ya kijamii katika Shuke yetu hii ya Liwiti" Said Side

Kupitia maadhimisho haya ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala amempongeza Mhe. Rais kwa kuendelea kutekeleza Miradi ya amaendeleo katika Wilaya ya Ilala, 

" Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala tunampongeza sana Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza Miradi ya Maendeleo katika Wilaya yetu ya Ilala tunaona Ujenzi wa Vituo vya Afya, Ujenzi wa Ujenzi wa Shule Mpya za Sekondari pamoja Ujenzi wa Madarasa ya Msambao Pochi la Mama katika Shule zetu za Sekondari" Alisema Said Side.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI