Header Ads Widget

BILIONI 13 KUTUMIKA KUJENGA VIVUKO VITATU VIPYA.

 




NA CHAUSIKU SAID _MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.



MKuu wa Mkoa wa Mwanza Adamu Malima amezindua ujenzi wa vivuko vitatu vya Nyakarilo - Kome, Bwiru - Bukondo na Ijinga - kahangala  ambavyo vitatoa huduma katika Wilaya ya Ukerewe na Buchosa vitakavyo gharimu kiasi Cha Sh, Bil 13.


Malima ameeleza kuwa kuanza utekelezaji wa ujenzi wa vivuko hivi ambavyo vitakapokamilika vitaondoa kero za usafiri Kwa wananchi wa maeneo husika.


"Niwatake wahusika wote kuhakikisha ujenzi huu unakamilika Kwa wakati na Kwa  viwango vya hali ya juu ili kutimiza azma ya serikali kuwaondolea kero wananchi na kuwaletea maisha Bora" Alisema Malima.



Ludovick Nduhiye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ameeleza kuwa Serikali kupitia Wizara ya ujenzi na uchukuzi imekuwa ikisimamamia ujenzi wa ukarabati wa vivuko pamoja na miundombinu yake kupitia wakala wa ufundi na umeme Tanzania (TAMESA)


"Kama alivyoeleza mtendaji  mkuu wa TEMESA katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 wakala unatekeleza ununuzi wa vivuko vipya nane (8), ukarabati wa vivuko 14 na miundombinu ya vivuko katika maeneo 11" Alisema Nduhiye.


Ameeleza kuwa serikali imekuwa na jukumu la kumwezesha wakala wa fedha za utekelezaji wa miradi hiyo Hadi kufikia mwezi Januari 2023 jumla ya Sh Bil, 15.6 zimekwisha tolewa kufanikisha utekelezaji miradi.


Ameeleza kuwa vivuko hivyo ambayo vimezinduliwa vimekuwa ni hitaji kubwa Kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ambayo vivuko vinaenda kutoa huduma baada ya ujenzi wake kukamilika.



" Ni mategemeo ya wizara Kwa wananchi katika maeneo husika watatumia fursa hii ya kuimarishwa na usafiri kuimarisha shuhuli zao za kiuchumi"Alisema Nduhiye.


Kwa upande wake Mtendaji Mkuu TEMESA Lazaro Kilahala ameeleza kuwa ujenzi wa vivuko vipya nane (8) kisorya - Rugenzi, Bwiro- Bukondo, Nyakarilo - Kome, iginja - Kahangala na Mafia - Nyamisati yenye thamani ya sh Bil 33.2 imeishaini.


Kilahala ameeleza kuwa serikali kupitia TEMESA  inafanya ukarabati wa vivuko 14 Kwa gharama ya Sh, Bil 22.99 na ukarabati wa miundombinu ya vivuko katika maeneo 11 Kwa gharama Sh Bil, 4.1 mikataba yenye thamani ya jumla ya Sh, Bil 60.3.


Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Songoro Marine Meja Songoro ameeleza kuwa watahakikisha vivuko hivyo vinakamilika muda muafaka ifika julai 2023 kama walivyokubalina na TEMESA.



Aidha Meja amemshukru Rais Dkt Samia Kwa kuendelea kuwaamini na kuwapa miradi mbalimbali ya kinaendelea wakandalasi wazawa.


Hata hivyo Kwa upande wao Wabunge wa maeneo hayo wameeleza kuwa kukamilika kwa vivuko hivyo vitasaidia uchumi wa wananchi wa maeneo hayo kukua, kupata kipato Cha kujitosheleza pamoja na kupata Kwa ukaribu huduma mablimbali za kijamii kupatikana kiurahisi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI