Header Ads Widget

UVCCM MOSHI VIJIJINI WAJA NA MIKAKATI.

 


Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP MOSHI.


Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM ) wilaya ya Moshi Vijijini umeanza harakati katika kuhamasisha vijana kujitokeza kwenye maadhimisho ya miaka 46 tangu kuzaliwa kwa CCM.


Maadhimisho hayo ambayo yanatajwa kuwa ya kipekee mwaka huu yataenda sanjari na kuwaeleza wananchi kile kilichofanywa na CCM lakini pia wanataraji kuwafanyia nini wananchi.


Mwenyekiti wa umoja huo wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima anasema kuwa maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika januari 26.2023 katika viwanja vya CCM mji mdogo wa Himo.

 

"Tunaendeleza tulipoishia, Zege alilali. KAZI indelee"anaeleza mwenyekiti huyo Kwa waandishi wa habari


Hata hivyo mwenyekiti huyo anasema tayari maandalizi yote yameshakamilika na kuwa wanataraji kuwa na wageni mbalimbali kutoka nje na ndani ya wilaya.


'Ivan Moshi ambaye ni mwenyekiti wa UVCCM mkoa naye atashiriki ambaye pia ni mgeni rasmi hivyo niwaombe wadau,wanachama na wapenzi wa chama chetu wajitokeze kwa wingi siku hiyo"anasema


Anasema kwa sasa wananchi hawahitaji maneno ya porojo na inatakiwa vitendo jambo ambalo CCM kwa muda wote imekuwa ikisimamia na kuwa matokeo chanya yanaonekana hivi sasa.


"Muda wa porojo umekwisha sasa tunaenda kusema tulichokifanya au tunafanya nini waache hao wengine wazunguke tu na maneno hapa hakuna mbambamba ni mwendo wa kazi tu"anasema


Mjumbe wa mkutano mkuu wilaya ya Moshi Vijijini kupitia CCM Wakili Emmanuel Mlaki anasema maadhimisho ya mwaka huu yanaenda kuonesha dira mpya kwa wananchi na kuwa ni mwendo wa vitendo.


"Wasije kudhani tunafanya siasa za maneno maneno huko tayari tulishahama tunaenda kuzungumza hoja zenye mashiko kwa  wanachama lakini pia kwa watanzania wote"anasema


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI