Mchungaji wa kanisa la NENO LA UNABII Iringa Yohana William amesema mlango pekee uliobaki kwa nchi ya Tanzania ni mlango "MACHOZI"
Nabii huyo amesema maana ya mlango wa machozi kama alivyosema ni mlango wa maombi, kwa maana hiyo inawapasa watanzania kuomba sana kwa Mungu ili waweze kusamehewa dhambi ili taifa ili lisiangamie.
Amesema kuwa uovu huwa unaenda kizazi mpaka kizazi kama hajatokea mtu atakayeonyeshwa maono juu ya uovu huo na kutubu ili yasitokee maangamizi, anasema yeye alionyeshwa maono hayo mwaka jana alipokuwa kwenye maombi, alipoambiwa kuwa uovu umekuwa kama bahari yaani umekuwa mwingi kwa Tanzania na ameambiwa apaze sauti ili watu waweze kutubu.
Amesema ni wajibu wa kila mtanzania aogope juu ya yale yatakayokuja kutukia juu ya taifa ili endapo watu hawatotubu, inatakiwa watu waombe pasipo kujali vyeo, uwezo, wala itikadi ili Mungu aweze kulisamehe taifa hili.
Mchungaji amekumbusha kwenye biblia habari ya maagizo aliyopewa Yona juu ya Ninawi ambapo watu wale walinusurika kwa kuwa walitii agizo lile. Hivyo basi yapasa watu watii maono haya hili Tanzania isiangamie,
Amesisitiza jambo ili lapaswa kutimizwa kwa watu wote bila kujali itikadi. Yapasa watu wote kuomba wao na familia zao na kwa umoja ili Mungu aweze kusamehe.
0 Comments