Chama cha mapinduzi (CCM)mkoa wa Iringa, Kimempongeza Rais wa Tanzania DR. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa .
Kuwa jambo hilo ni muendelezo wa ukuaji wa demokrasia hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi
(CCM) mkoa wa Iringa Daudi Yassin, wakati akizungumza na wanahabari mkoani hapa leo Ijumaa Januari 6,2023, na kuongeza kuwa ruksa ya kuanza kwa mikutano ya
hadhara kwa vyama vya siasa hapa nchini, isiwe chanzo cha vurugu wala uvunjifu
wa amani miongoni mwa watanzania.
Mwenyekiti huyo amesema baada ya ruhusa ya mikutano chama
cha mapinduzi mkoa wa Iringa kimejipanga vyema kuanza mikutano ya hadhara bila
hofu wala uoga kama inavyosemwa na baadhi ya ya wapinzani.
Katika hatua nyingine amevitaka vyama vingine kuitumia
vizuri fursa hiyo kwa kufanya mikutano yenye tija, kwa kuzitangaza sera na
mipango ya vyama vyao kwani wao watakwenda kuwatangazia wananchi juu ya
utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ambayo ndiyo inaongoza nchi kwa
sasa.
Hata hivyo amekanusha madai ya kuwa kipindi mikutano ya
siasa imezuiliwa hapa nchini, chama cha
mapinduzi (CCM) kiliendelea mikutano
hiyo kama kawaida na kusema kilichokuwa kinafanyika ni ukaguzi wa ilani pekee
na siyo mikutano ya hadhara kama inavyodhaniwa.
0 Comments