Header Ads Widget

RC NJOMBE ATAKA WAZAZI AMBAO HAWAJAWAPELEKA SHULENI WATOTO KUKAMATWA NA KUFANYISHWA USAFI KWENYE SHULE NA VITUO VYA AFYA




********

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Mkuu wa Njombe wa Njombe Antony Mtaka amemuagiza mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kuwakamata wazazi wote ambao hawajapeleka watoto kuanza muhula mpya wa masomo hadi sasa na kuwafanyisha usafi kwenye shule hizo pamoja na vituo vya afya badala ya kuwaweka rumande.

Mtaka ametoa agizo hilo akiwa katika shule ya Sekondari Mbeyela mjini Njombe wakati akikagua zoezi la uripotiji wanafunzi shuleni ambapo katika shule hiyo wameripoti wanafunzi 62 pekee kati ya 300 wa kidato Cha kwanza wanaopaswa kuanza masomo.

Aidha Mtaka amesema hakuna sababu ya kuwapeleka rumande wazazi hao wakamalize chakula Cha serikali hivyo wanapaswa kufanya usafi kwani haiwezekani serikali ikajenga madarasa na kufuta ada halafu wazazi washindwe kuwapeleka watoto shuleni.

Mkuu wa shule ya Sekondari Mbeyela Mwalimu Jimmy Ngumbuke amesema kasi ya wanafunzi kuripoti shuleni ni ndogo na hivyo jitihada zaidi zinahitajika kwa wazazi.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Njombe KISSA KASONGWA amekiri kupokea maelekezo ya mkuu wa mkoa na kwenda kuyafanyia kazi kikamilifu

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI