Header Ads Widget

TAASISI ZA SERIKALI KUPITISHWA KWENYE MFUMO WA UKUSANYAJI WA MAPATO WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA



Na Angela Msimbira, OR-TAMISEMI


Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetekeleza agizo la Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) la kujengea uelewa kuhusu matumizi ya Mifumo kwa Taasisi zinazofanya kazi na Wizara hiyo.


Hayo yamebainishwa jana Januari 9,2023 na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya TAMISEMI, Ramadhani Kailima wakati akifunngua mafunzo ya siku tano kuhusu utekelezaji wa Mfumo wa ukusanyaji wa Mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wa LGRCS na TAUSI yaliyofanyika Jijini Dodoma.


Amezitaja Taasisi hizo kuwa ni Ofisi ya Mashitaka, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mamlaka ya Serikali Mtandao (Ega), Polisi , Wizara ya Fedha, Ofisi ya Waziri Mkuu na Tume ya Utumishi wa Umma


Amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Mfumo wa ukusanyaji wa mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGRCS) ambao unaenda kufungwa na mfumo wa TAUSI ambao unaenda kuanza kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo mpaka sasa Halmashauri 54 zimeanza kuutumia Mfumo huo.


Kailima amefafanua kuwa uelewa wa pamoja wa utumiaji wa mifumo ya TEHAMA katika ukusanyaji wa mapato utasaidia ufuatiliaji, ukaguzi, uchunguzi, kufungua mashitaka na kuiwezesha Serikali kuwa na ushahidi wa kutosha utakaowezesha kupeleka mashitaka na kuwezesha kuchukua hatua stahiki kwa watakaotuhumiwa kukiuka taratibu na miongozo ya ukusanyaji wa mapato kupitia mifumo ya ukusanyaji wa mapato iliyoanzishwa.



Ameeleza kuwa mafunzo hayo yatawawezesha kusikiliza hoja na kuweza kutoa maoni jinsi ya kuboresha mifumo hiyo lengo ni likiwa ni kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa kufuata sheria na taratibu za fedha


Naye Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Erick Kitali ameeleza kuwa tangu mwaka 2014/2015, Ofisi ya Rais TAMISEMI ilianza kutumia mifumo ya Kielekroniki katika kukusanya Mapato ambao ulikuwa ukijulikana kama Local Government Revenue Collection System (LGRCS) na umetumika kwa muda wa miaka saba..




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI