NA AMINA SAIDI,MATUKIO DAIMA TANGA
Mkuu wa mkoa wa Tanga Omary Mgumba ametangaza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa miaka miwili ambapo alisema wamepokea zaidi sh.bilion 95 kwa ajili ya uboreshaji wa sekta ya Elimu kutoka kwa Dkt.Samia suluhu Hassan.
Akizungumza katika Kongamano la kutangaza mafanikio ya serikali ya Awamu sita ndani ya miaka miwili iliyofanyika katika ukimbi wa Legal Naivera alisema wamefanikiwa kujenga zaidi ya madarasa mapya 16 na madarasa 327 kupitia fedha iliyoletwa na serikali ya awamu ya sita chini ya usimamizi wa Dkt Samia suluhu Hassan.
Aidha alisema madarasa hayo 16 na madarasa 327 yote yamepokea wanafunzi,lakini pia kupitia fedha hizo wamefanikiwa kujenga mabweni zaidi ya 21na matundu ya vyoo 1774 na nyumba za waalimu 4.
Sambamba na hayo mkuu wa mkoa huyo alieleza kuwa Mapato katika Halmashauri zimeongezeka kutoka billion 29 ya mwaka 2021 hadi kufikia billion 35 mwaka 2022.
Aliongeza kusema kuwa sababu za kutangaza mafanikio hayo ni kutokana na taarifa mbalimbali ya upotoshaji inayovuma mtandaoni ya kwamba serikalj haijafanya jambo lolote hivyo kupitia taarifa hiyo wananchi wamejua kuwa serikali imefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga Ustad Rajabu Abdarahman Abdalah alisema kuwa hayo mafanikio ya serikali ya awamu ya sita ni utekelezaji wa ilani ya chama hicho chini mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Sambamba na hayo aliwakemea wahudumu wa afya ambao wanahatibh trauma yao kwa kutumia lugha mbaya kwa wagonjwa wakati wakuwapatia huduma.
0 Comments