Header Ads Widget

RC-LINDI ATAKA BARABARA YA HOTELITATU - PANDE ITUMIKE MWAKA MZIMA

 


NA HADIJA OMARY,MATUKIO DAIMA,

LINDI

MKUU wa Mkoa wa Lindi, Bi. Zainab Telack amewataka wakala wa barabara za vijijini na mijini TARURA  Wilayani Kilwa Mkoani Lindi kumsimamia mkandarasi wa kampuni ya MS ERIT INVESTIMENT GROUP LIMITED anaetekeleza mradi Barabara ya hotelitatu – pande kwa urefu wa kilometa 14 anamalizia kasoro ndogondogo zilizopo kwenye Barabara hiyo  akiwa katika kipindi cha matazamio ili iweze kutumika kwa muda mrefu.

 

Bi Zainab ameto agizo hilo leo January 22, 2023 alipotembelea na kukagua  barabara hiyo na kubaini baadhi ya kasoro ambazo amesema endapo zisiposimamiwa kikamilifu na kufanyiwa marekebisho  lengo la Serikali  kuwaondolea changamoto wananchi wa maeneo hayo hayatakamilika.

 

“hii Barabara inatakiwa ipitike mwaka mzima na kama Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara na tumeweka kifusi kwa gharama kubwa niwatake  TARURA kuisimamia hii barabara ninyi ndio wataalamu mnajua cha kufanya msimamieni mkandarasi ili iweze kupitika kwa mwaka mzima”.

 


Telack amesema kwa kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo asingependa kuendelea kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi.

 

“Wananchi wakilalamika maana yake kuna mapungufu sasa rekebisheni mapungufu hayo barabara hii ipitike, kwa kuwa sasa mvua zinanyesha kukikauka kidogo mkandarasi arudi site akate hiyo mitaro inayotakiwa ili maji yasilale barabarani” alisema Telack

 

Kwa upande wake kaimu meneja wa TARURA Wilayani Kilwa Mhandisi David Geofrey alisema kuwa  mradi huo wa Barabara  ambayo ni kilometa 10 kutoka Mkazambo - pande na kilometa 4 kutoka Mkazambo -  Lihimilo ulianza utekelezwaji wake febduary 7 /2022  na kukamilika august 31/2022 umeghalimu kiasi cha shilingi milioni 500   zilizotokana na Tozo ya mafuta.

Alisema baada ya mradi huo kukamilika kwa sasa mkandarasi yupo katika kipindi cha matazamio kabla ya mradi huo kuukabidhi rasmi ambapo kasoro zinazojitokeza kwa wakati huu mkandarasi huyo atatakiwa kuzifanyia kazi.

 

Hata hiyo Mhandisi Geofrey alisema kuwa ili kufanya marekebisho katika kasoro hizo ndogo ndogo ikiwa pamoja na kuchimba mifereji tayari TARURA wameshamuandikia barua mkandarasi anaetekeleza mradi huo ya kumtaka arudi katika eneo la mradi (site) kwa ajili ya kufanya marekebisho hayo

 

Wakizungumza na MATUKIO DAIMA  baadhi ya wananchi wa Kijiji hiko akiwemo Diwani wa kata ya Pande Selemani Waziri  waliiomba serikali kufanya marekebisho ya haraka katika barabara hiyo sambamba na kumalizia kujenga kipande cha barabara kilichobakia ili waweze kutumia barabara hiyo kwa uhakika

Alisema   kuwa miongoni mwa changamoto wanayokabiliana nayo wakazi wa Kata hiyo hasa wakati wa masika ni kushindwa kusafirisha mazao yao kunakotokana na kukosa miundombinu ya Barabara ya uhakika.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI