Naibu waziri wa usafirishaji na uchukuzi Mh. Mhandisi Godfrey Kasekenya amempongeza mkandarasi wa uwanja wa ndege wa Iringa kwa kuendelea kufanya kazi ndani ya wakati.
Kasekenya ameyasema hayo leo alipotembelea mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa iringa ambao mwanzo uliitwa uwanja wa nduli ambao ni uwanja mmojawapo wa kimkakati kusini mwa Tanzania kwa ajili ya kukuza biashara na uchumi.
Naibu waziri huyo amesema kukamilika kwa uwanja wa ndege huo utafungua fursa za uwekezaji na kupanua fursa zilizopo kama kilimo na utalii.
Katika hatua nyingine, Kasekenya amewataka wawekezaji wawe tayari kujenga miundombinu wezeshi kwa ajili ya kujenga uchumi imara.
Kwa upande wake Meneja wa TANROADS mkoa wa Iringa Mhandisi Daniel Kindole amesema, uwanja wa ndege wa iringa utatumika usiku na mchana kwa sababu wamejipanga kufunga taa zitakazosaidia shughuli mbalimbali uwanjani.
Uwanja huo uliozinduliwa Agosti mwaka jana kwa ajili ya ukarabati na upanuzi na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dakta Samia Suluhu Hassan na unaokadiliwa kukamilika Agosti mwaka huu mpaka sasa umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 43 ikiwa ni ongezeko kutokana na upasuaji wa mwamba kutoka bilioni 21 zilizotolewa mwanzo.
0 Comments