Header Ads Widget

MWENYEKITI WA UWT MBINGA AWATAKA WANAWAKE KUZIENZI KAZI ZINAZOFANYWA NA CCM.

 

Mwenyekiti UWT Wilaya ya Mbinga Grace Millinga
Katibu wa UWT Wilaya ya Mbinga

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

 Na Amon Mtega, Mbinga.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya  Wanawake (UWT) wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Grace Millinga amewataka Wanawake wa  Wilaya hiyo kuendelea kuzienzi kazi mbalimbali zilizofanywa na Chama hicho ikiwemo kuilinda Amani iliyopo.


Millinga ametoa wito  huo wakati akizungumza na baadhi ya Wanawake wa tawi la CCM lililopo Kijiji cha  Lipumba kata ya Kihangimahuka Wilaya ya Mbinga  katika kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya  kumbukizi ya kuanzishwa kwa chama cha mapinduzi CCM ambapo kilele chake ni Februari tano mwaka huu.


Mwenyekiti huyo amesema kuwa tangu CCM ishike madaraka(Dola) imefanya maendeleo mbalimbali kwa Wananchi hivyo ni vema Wananchi wakaendelea kuzienzi kazi hizo pamoja na kukipatia ridhaa chama hicho.


 Millinga akizungumza huku akielezea kazi zilifanywa na Serikali kupitia CCM ikiwemo Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amesema ni kazi ambazo zinaonekana hata kwa macho jambo ambalo amedai kuwa ni lakujivunia.


Aidha katika hatua nyingine mwenyekiti huyo akiwa ameongozana na kamati ya utekelezaji ya UWT ya Wilaya pamoja na baadhi ya madiwani wa vitimaalumu wamefanya shughuli mbalimbali za kijamiii ikiwemo usafi kwenye maeneo ya ofisini za chama na maeneo ya umma.


 Hata hivyo kiongozi huyo ameongoza zoezi la kuhakikisha Wanawake wa Wilaya hiyo wanazisajili kadi zao za Jumuiya na Chama kwa mfumo wa Kilektroniki (Tehama)ili kila mwanachama aweze kuwa na kumbukumbu sahihi zilizowekwa kwenye mfumo wa kisasa.


 Kwa upande wake katibu wa UWT Wilaya ya Mbinga Elimina Makiya amesema kuwa zoezi la kujisajili kwa wanachama ili kupatiwa kadi za kisasa linaendelea vizuri na kuwa mkakati ni kuhakikisha Jumuiya ya Wanawake inakuwa na wanachama wengi.


 Katibu Makiya amesema kuwa Jumuiya hiyo haitamvumilia mtendaji ambaye  anataka kukwamisha zoezi hilo kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwakosesha haki ya Msingi wanachama.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS