Header Ads Widget

MWENYEKITI UVCCM MWANGA AISHA MFAUME AWATAKA VIJANA KUACHA KULALAMIKA.

 


Na WILLIUM PAUL, MWANGA.

VIJANA nchini wametakiwa kuacha tabia ya kulalamika badala yake wachangamkie mikopo inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri kujinufaisha pamoja na kujipatia ajira ya kujiajiri.



Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Aisha Mfaume wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi ambapo vijana hao waliazimisha kwa kupanda miti kata ya Msangeni na kukagua miradi ya Serikali na chama.



Alisema kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani imetoa fedha nyingi ambazo ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ya kila Halmashauri kwa ajili ya kukopesha mikopo isiyo na riba kwa makundi maalum ya Vijana, wanawake na watu wenyeulemavu na kuwataka vijana kuunda vikundi na kukopa fedha hizo.



"Vijana tunapaswa kuacha kulalamika kwa kukosa ajira badala yake tuchangamkieni mikopo hii isiyo na riba kwa kuitumia kama fursa ya kujiajiri sisi wenyewe na kujipatia maendeleo hili linawezekana kabisa tuundeni vikundi kwa wingi na kuvisajili" alisema Aisha.



Mwenyekiti huyo wa Uvccm Mwanga alitumia pia nafasi hiyo kuwataka vijana kuepukana na majukumu na badala yake wapendani na kufanya kazi kwa ushirikiano na mshikamano mkubwa.



Alisema kuwa, kwa sasa uchaguzi ndani ya chama umekwisha hivyo ni jukumu la kila mwanachama kuvunja makundi yote ndani ya chama kwani makundi yamekuwa yakisababisha mpasuka na mafarakano.



"Vijana uchaguzi umepita na viongozi wa Chama na Jumuiya zake tumeshawapata sasa nijukumu letu kila mmoja kuvunja makundi ili kubakiwa na kundi moja la Chama cha Mapinduzi na tuendelee kukipigania chama chetu kiendelee kuongoza kuanzia viongozi wa vitongoji, vijiji, kata, wilaya na hata Taifa" alisema Aisha.

Aidha alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hasani kwa jinsi ambavyo ametoa fedha nyingi za miradi mbalimbali katika wilaya ya Mwanga na kuwataka vijana kuzisemea kwa wananchi kazi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS