Header Ads Widget

MIGAMBO KUKAMATA WAZAZI WASIOPELEKA WATOTO SHULE WANGING'OMBE NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Zikiwa zimepitia siku tatu tangu kuanza kwa muhula mpya wa masomo wa mwaka 2023 jumla ya wanafunzi 260 hawajaripoti shuleni kuanza masomo yao katika shule ya sekondari Igima wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe.


Akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya zoezi la uandikishaji wanafunzi katika shule hiyo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Agnetha Mpangile akiongozana na kamati ya huduma za jamii ya halmashauri hiyo amebaini kuwapo kwa idadi ya wanafunzi hao ambao hawajafika shule hadi sasa huku akimuagiza afisa mtendaji kutumia migambo wake kuwakamata wazazi ambao hawajapeleka watoto shule pamoja na kuwataka wanafunzi waliopo kusoma kwa bidii.


Awali mkuu wa shule ya sekondari Igima Mwalimu Godfrey Mwalongo amesema endapo wanafunzi wote wataripoti shuleni hapo watafika zaidi ya 900 huku idadi ya walimu ikiwa bado ni changamoto hususani katika masomo ya Sayansi.



Kwa upande wake kaimu afisa mtendaji wa Kata ya  Igima Godwin Swalle amesema anakwenda kuchukua hatua stahiki dhidi ya maelekezo ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe pamoja na yale aliyoyatoa mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka.


Aidha mwenyekiti wa kamati ya huduma za Jamii halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe na diwani wa Kata ya Wangama Fredrick Mwalongo amewataka wanafunzi hao kuzingatia nidhamu katika masomo yao.



Kituo hiki kimezungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Igima akiwemo Oliver Kidenya,Maya Mng'ong'o na Nimrod Makweta ambao wanakiri kuwa ujio wa wageni mbalimbali shuleni hapo kunawaongezea molari ya kusoma.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI