Header Ads Widget

MBUNGE WA MADABA DKT MHAGAMA AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI YA AWAMU YA SITA.

 

Mbunge wa Jimbo la Madaba Dkt Joseph Mhagama akiweka jiwe la msingi katika ofisi inayojengwa kwenye Kijiji cha Wino.
Mbunge Dkt Joseph Mhagama akifyatua tofari la saruji katika Kijiji cha Igawisenga kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba ya mwalimu katika shule ya Msingi kijijiini hapo.

xxxxxxxxxxxxxxxxxx

 Na Amon Mtega, Madaba.

MBUNGE wa Jimbo la Madaba Mkoani Ruvuma  Dkt Joseph Mhagama amewataka wakazi wa Jimbo hilo kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara .


Mbunge Dkt Mhagama ametoa wito huo wakati akizungumza na Wananchi wa kata ya Wino  alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye Jimbo hilo.


Dkt Mhagama akizungumza na Wananchi hao amesema kuwa kuwa mafanikio yote ya maendeleo yanayofanyika katika Jimbo hilo ni kutokana na ufanyaji kazi wa Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hivyo kazi ya Wananchi ni kuunga mkono kazi hizo.


Mbunge huyo akiwa kwenye ziara hiyo ambayo ameambatana na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Songea Vijijini Thomas Msolwa pamoja na mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Theofanes Mlelwa kama Wananchi wakaendelea kutambua kazi zinazofanywa na Serikali watambue kuwa maendeleo yatazidi kusongambele kwenye Jimbo hilo.


Akiwa katika moja ya miradi hiyo ikiwemo wa ujenzi wa Nyumba ya mwalimu katika shule ya Msingi Igawisenga kata ya Wino amesema kuwa amejionea kazi inaenda vizuri kuwa nyumba hiyo ikikamilika itawafanya walimu kuishi kwenye mazingira bora.


Hata hivyo Mbunge huyo amechangia sh.Milion tisa pamoja na kuweka jiwe la msingi katika kufanikisha ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Wino ambayo hadi kukamilika kwake itagharimu zaidi ya Sh.Milion 80 ambazo asilimia kubwa ni nguvu za Wananchi.


Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa Nyumba ya mwalimu katika shule ya Msingi Igawisenga Afisamtendaji  wa Kijiji hicho Jesca Haule amesema ujenzi wa Nyumba hiyo utagharimu sh.Milion 50 ambayo fedha hiyo imetolewa na Serikali kuu na hakuna mchango wa mwananchi.


Mtendaji huyo akitoa taarifa hiyo mbele ya Mbunge huyo amesema kuwa licha ya ujenzi wa Nyumba hiyo lakini bado Kijiji hicho kimepatiwa miradi mbalimbali Serikalini pamoja na miradi mingine jitihada za Mbunge wa Jimbo hilo Dkt Joseph Mhagama.


Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba Theofanes Mlelwa ambaye pia ni diwani wa kata ya Wino amesema kuwa Halmashauri kupitia Mbunge huyo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali kwenye Jimbo hilo na kuwafanya Wananchi waendelee kunufaika.


Mwenyekiti Mlelwa amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopitia vijiji vingi kwenye jimbo hilo havikuwa na maji ya uhakika ,umeme,barabara ,na baadhi ya shule kuwa na majengo chakavu ,lakini katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita yote yameenda kwa kasi sasa huduma hizo zipo karibu vijiji vyote vya Jimbo hilo kama kunamaeneo ambayo bado basi ni asilimia chache sana.


Hata hivyo mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Songea Vijijini Thomas Msolwa amesema kuwa Chama hicho bado kinaendelea kusimamia utekelezaji wa ilani hivyo amewaomba Wananchi kuendelea kuiamini Serikali yao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI